EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, December 24, 2013

UFARANSA KUJIPIMA NGUVU MECHI TATU KABLA YA KWENDA BRAZIL.

TIMU ya taifa ya Ufaransa inatarajiwa kuchezwa mechi tatu za kimataifa za kirafiki kabla hawajaondoka kuelekea nchini Brazil kushiriki michuano ya Kombe la Dunia. 
Shirikisho la Soka la nchi hiyo limedai kuwa timu hiyo itacheza mchezao wake wa kwanza wa kirafiki huko Stade de France mei 27 huku michezo mingine ikichezwa katika miji ya Nice Juni mosi na Lille Juni 8. 
Majina ya timu watakazopimana nazo nguvu yanatarajiwa kutolewa mapema mwakani. Ufaransa imepangwa kundi F sambamba na timu za Switzerland, Ecuador na Honduras.

 

 

 PETROVA AJITOA AUSTRALIA OPEN.

MCHEZAJI nyota wa tenisi, Nadia Petrova wa Urusi amejitoa katika michuano ya wazi ya Australia inayotarajiwa kuchezwa mapema mwakani kufuatia kifo cha mama yake kilichotokana na ajali ya gari. 
 
Mama yake Petrova aitwaye Nadezhda Illyina alikuwa mwanariadha ambaye aliwahi kushinda medali ya shaba katika mbio za mita 400 kupokezana vijiti katika michuano ya olimpiki iliyofanyika jijini Montreal mwaka 1976.
 
 Mrusi mwenzake Maria Kirilenko ambaye anashika namba 19 katika orodha za ubora duniani naye amjitoa kutokana na majeruhi.
 
 Kujitoa kwa Petrova kunamaanisha kuwa Tsevetana Pironkova mwenye umri wa miaka 26 raia wa Bulgaria atachukua nafasi hiyo katika droo kubwa ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment