MACHO na masikio ya
mamilioni ya mashabiki wa soka Ijumaa hii yatahamia katika kiota cha
Costa do Sauipe kilichopo katika jimbo la Bahia nchini Brazil kushuhudia
upangwaji ratiba ya michuano ya Kombe la Dunia 2014.
Shirikisho la Soka
Duniani-FIFA limetenga kiasi cha dola milioni nane kwa ajili ya
shughuli hiyo itakayoonyeshwa dunia nzima kwa dakika 90 huku
ikishirikisha nyota wa soka wa Brazil pamoja na muziki utakaowapa ladha
mashabiki.
Baadhi ya nyota wa zamani katika soka wakiwemo Pele, Zinedine
Zidane na Lothar Matthaeus watakuwepo kusaidia uapngwaji ratiba hiyo
wakati maofisa 5,000, waandishi wa habari na wageni waalikwa watakuwa
wakishuhudia tukio hilo muhimu.
Brazil imesubiri kwa miaka 64 kuandaa
michuano hiyo baada ya kushindwa kunyakuwa kombe hilo mwaka 1950 katika
mchezo wa fainali dhidi ya majirani zao Uruguay katika Uwanja wa
Maracana jijini Rio de Janeiro.

No comments:
Post a Comment