![]() |
| BAndari ya Dar es salaam |
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa tatu wa masuala ya usafirishaji wa majini na nchi kavu kwa nchi za Afrika.
Ulinzi na usalama wa vyombo vya usafirishaji majini pamoja na ufanisi wa bandari wa Dar es Salaam ni mojawapo ya mada zitakazojadiliwa katika mkutano huO.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Zacharia Mganilwa, amesema mkutano huo utafanyika kwa siku mbili kuanzia kesho na kesho kutwa.Mganilwa amesema NIT, Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) Pamoja na
Shirika lisilo la Serikali la Ujerumani Kuhne-Stiftungi, ndiyo waandaaji wa mkutano huo utakaowakutanisha wadau wa usafirishaji kutoka Bara la Ulaya, Amerika, na Afrika kujadili masuala hayo. Amesema sekta ya Uchunguzi ni mojawapo ya sekta saba zilizopo katika mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa (BRN) hivyo kuna haja ya bandari ya Dar es Salaam kupewa kipaumbele katika kuinua uchumi wa nchi.


No comments:
Post a Comment