Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linapanga kupambana sasa na waasi wa Kihutu kutoka Rwanda walioko katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa serikali ya Kongo amesema hayo leo na kuongeza kuwa hakuna nafasi tena nchini humo kwa jeshi ambalo si rasmi.
Mende amesema kuwa kundi la waasi la M23 ambalo limeshindwa, limekuwa katika orodha ya juu kabla ya kusalimu amri leo.
Mende amesema kuwa nafasi ya kundi hilo imechukuliwa sasa na kundi la waasi la FDLR , na sasa ni zamu ya kundi hilo kunyang'anywa silaha.Msemaji huyo wa serikali amesema kuwa hatua za kijeshi zitachukuliwa katika mapambano ambayo yatafanywa na jeshi la nchi hiyo, dhidi ya vikundi mbali mbali vyenye silaha katika eneo la mashariki ya nchi hiyo.


No comments:
Post a Comment