Nigeria imetaka
kufanywa marekebisho katika muundo wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Rais Goodluck
Jonathan wa Nigeria amesisitiza juu ya ulazima wa kufanyiwa marekebisho muundo
wa mahakama ya ICC, na kueleza kuwa nchi yake haitajiondoa katika chombo hicho
cha kimataifa, licha ya nchi za Kiafrika kubainisha wasiwasi wao kuhusu
utendaji wa mahakama hiyo.
Rais wa Nigeria
ameongeza kuwa nchi yake itafanya juhudi kwa kushirikiana na nchi nyingine ili
kuiimarisha mahakama ya ICC.
Rais Goodluck
Jonathan ambaye aliyasema hayo huko Abuja mji mkuu wa Nigeria, wakati
alipokutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai
yenye makao yake huko Hague Uholanzi, ameongeza kuwa mahakama hiyo inapaswa
kutafuta ufumbuzi wa masuala mbalimbali na si kuyafanya masuala hayo kuwa
magumu zaidi.
Rais Goodluck
Jonathan amesema mahakama ya ICC inapasa kutambua matatizo ya viongozi wa nchi
za Kiafrika na kutilia maanani wasiwasi wa viongozi hao.

No comments:
Post a Comment