Kumekuwepo na misururu ya milipuko
midogo nje ya ofisi za kimkoa za chama tawala cha Kikomunisti nchini China na
kusababisha kifo cha mtu mmoja
Maafisa wa polisi katika eneo hilo
wamesema kuwa milipuko hiyo ilisababishwa na mabomu madogo yaliyotengenezwa
nyumbani.
Mlipuko hiyo iliotokea muda wa
asubuhi wenye shughuli nyingi, ilisababisha kuvunjika kwa madirisha na moshi
mkubwa kufuka.
Ripoti zilizotolewa na shirika la
habari la serikali zilisema kuwa mabomu madogo yalikuwa yamefichwa ndani ya
maua kando ya barabara.
Milipuko hiyo imetokea Kaskazini mwa
China katika eneo la, Tai-yuan, mkoani, Shanxi,Taarifa za vyombo vya habari nchini
humo vinasema kuwa watu 8 wamejeruhiwa na magari mawili kuharibiwa.

No comments:
Post a Comment