EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, November 6, 2013

KITUO CHA UWEKEZAJI NCHINI (TIC) CHAWASHAURI WAWEKEZAJI KUGEUKIA SEKTA NDOGONDOGO

Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kimewashauri wawekezaji wa ndani na nje kutumia fursa kinazozitoa kwa wawekezaji  kuwekeza katika sekta ndogo ya zao  la korosho ili kuongeza uzalishaji wake.
 
Mkurugenzi wa TIC-Juliet Kairuki

Mkurugenzi Mtendaji  wa kituo hicho, Juliet Kairuki, amesema hayo jana wakati wa mkutano wa wadau wa sekta hiyo, na kuongeza kuwa wanahitajika kukitumia kituo hicho ili kupata fursa zitakazowawezesha kuwekeza  zaidi katika uzalishaji wa zao hilo. Amesema TIC imeweka vivutio mbalimbali kwa wawekezaji ambao wamejizatiti kuwekeza katika kilimo, ikiwamo misamaha ya kodi kwa bidhaa za mitaji.Ameongeza kuwa Tanzania bado inahitaji wawekezaji kuwekeza katika kilimo cha zao hilo, viwanda vya kusindika na kuyatumia masoko ya ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake mchumi Mwandamizi Kitengo cha Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Aneth Mathania, amewaeleza wawekezaji kuwa Tanzania ina barcode yake, hivyo wakiwekeza katika zao hilo halitapata shida ya soko.

No comments:

Post a Comment