EBENEZA MARCH 9 2014

SWACO

royal

tt

NIMO

mvuto
Friday, October 18, 2013
WANAJESHI 57 WA KONGO WASHIKILIWA NA JESHI LA ANGOLA
Ofisa wa kijeshi wa serikali ya Kongo Brazzaville amesema kuwa, wanajeshi 57 wa nchi hiyo, wanashikiliwa na askari wa Angola katika sehemu ya mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Ofisa huyo wa kijeshi ambaye hakutaka kutaja jina lake, amewaambia waandishi wa habari wa shirika la habari la China Xinhua kuwa, wanajeshi hao walizingiriwa na askari wa Angola, wakiwa na silaha nzito karibu na kituo cha ukaguzi kilichoko katika mpaka wa sehemu ya Kusini Magharibi ya Kongo Brazzaville na kupelekwa katika mji mkuu wa jimbo la Cabinda nchini Angola.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la nchi hiyo, wanajeshi wanaoshikiliwa ni pamoja na maofisa watatu wa kijeshi, chanzo cha tukio hilo kinahusiana na mgogoro kati ya pande hizo mbili kuhusu mpaka.
Lakini balozi wa Angola nchini Kongo Brazzaville amekanusha na kusema mikwaruzano katika sehemu ya mpaka inatokea mara kwa mara, kati ya raia au kati ya majeshi la kulinda usalama mpakani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment