Wazazi na walezi katika Manispaa ya Mtwara Mikindani
wametakiwa kujenga mazoea ya kuwapeleka watoto wao kliniki kila tarehe
husika inapofikia, ili kujua ukuaji na
mabadiliko ya watoto wao.
![]() |
wanafunzi wakiwa ktk foleni ya uji |
Hayo yameelezwa na mtumishi wa zahanati ya Polisi
Ligula nesi Moshi Ahmed wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa pride fm
katika zahanati hiyo, ambapo amesema kuwa kwa kuwapeleka watoto kliniki kila
awamu itasaidia kujua mabadiliko ya afya ya watoto hao, jukumu ambalo
linatakiwa lifanywe kwa ushirikiano kati ya wazazi wa pande zote baba na mama.
Kwa upande wake mmoja wa mzazi Monika Hamisi amesema
kuwa kwa wale wazazi wenye imani potofu na kliniki ni kwenda kinyume na malezi
na haki ya mtoto, kwani kwa kwenda kilinik kutamwezesha mtoto kupimwa uzito,
kwa kujua ongezeko na upungufu wa uzito wa watoto na itasaidia kupunguza tatizo
la kupewa dawa tofauti na vipimo pindi atakapoumwa.
Mama Monika ameiomba serikali iongeze kliniki za
akina mama na watoto katika maeneo ya vijijini kwani kwa kufanya hivyo
itasaidia kupunguza safari ndefu wanazotumia akina mama kutembea kutafuta
huduma za afya ya mama na mtoto.
No comments:
Post a Comment