michuano
inayovikutanisha vyuo vya ualimu kanda ya kusini maalufu kama umisavuta ambayo
itaanza kutimua vumbi siku ya jumatatuya tarehe 21 october 2013 katika viwanja
vya chuo cha ualimu masandube na chuo cha ualimu mtwara kawaida ttc,
![]() |
UWANJA WA MICHEZO WA CHUO |
hatimaye maandalizi yake yamefikia tamati na
huku chuo cha ualimu masandube ambacho ni mwenyeji wa mashindano hayo
kikielezea kuridhika na hali ya maandalizi na kuwa wao kama wenyeji wako tayari
kwa michuano hiyo itakayochukua takribani wiki moja .
akitoa
taarifa ya jumla ya michuano hiyo mwl wa michezo wa chuo cha masandube barnabas mohuvone amesema kuwa vyuo
vinavyotarajiwa kushiriki michuano hiyo ni pamoja na chuo cha ualimu
kitangari,mtwara kawaida ttc,nachingwea, songea na masandube yenyewe.
huku
akitanabaisha michezo itakayovurumishwa katika michuano hiyo ambapo kwa upande
wa mpira kutakuwa na mpira wa miguu kwa wavulana,basket ball,volleybal,na
netball.
pia kutakuwa
na mbio fupi za mita 100,200,400,na 800 huku mbio za kati zikiwa ni za mita
1500. na katika michezo ya mitupo watahusisha mitupo ya kisahani,kurusha mkuki,
pamoja na kurusha tufe. na mwisho kabisa ni mchezo wa mruko ambapo mwaka huu
kuna aina moja tu ya mruko nao ni mruko wa chin.
No comments:
Post a Comment