EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, October 19, 2013

UMOJA WA MATAIFA WAINGILIA SUALA LA KUSHUKA KWA ELIMU



Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, wanafunzi wengi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, hawahudhurii masomo shuleni kutokana na kuongezeka kwa hali ya ukosefu wa amani katika nchi hiyo.
 
Katibu mkuu umoja wa mataifa Ban Ki moon

Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, kwa uchache asilimia 70 ya wanafunzi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati hawaendi shule tangu kuongezeka kwa machafuko katika nchi hiyo.
Taarifa ya UNICEF inaonesha kwamba, karibu asilimia 65 ya shule ambazo zimefanyiwa uchunguzi na Umoja wa Mataifa ama zimebomolewa, kukakaliwa kwa mabavu au vifaa vyake vimeporwa na waasi.




Taarifa hiyo ya Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) inaonesha kwamba, nusu ya taasisi na vituo vya elimu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati zimesitisha shughuli zake kutokana na ukosefu wa amani.
UNICEF imetahadharisha kwamba, maelfu ya watoto wanakabiliwa na hatari ya kufukuzwa shule kutokana na kutohudhuria shule kwa miezi kadhaa sasa. Jamhuri ya Afrika ya Kati imeendelea kushuhudia machafuko tangu serikali ya Rais Francois Bozize apinduliwe na muungano wa waasi wa SELEKA.
 

No comments:

Post a Comment