Tamasha hilo linaloshirikisha makabila
matatu maarufu toka mkoani mtwara yaani WAMAKUA,WAYAO na WAMAKONDE limezinduliwa rasmi hii leo katika
uwanja wa nangwanda sijaona mjini mtwara ikiwa ni siku ya kwanza ya maonyesho
hayo ambayo yatadumu kwa muda wa siku tatu toka kuanza kwake hii leo.
Uzinduzi hu ulioanza majira ya saa nne asubuhi na kumalizika
saa kumi na mbili jioni ulihusisha maonyesho mbalimbali ya sanaa za ngoma toka
kwa vikundi vya ngoma vya makabila husika ambapo makundi yaliyopata fursa ya
kuonyesha michezo yao leo ni kundi la Chipapayungu la kabila la
kimakonde,Sinzia toka kabila la wamakua Madudu pia toka kwa wamakonde Mselemba
toka katika kabila la wayao.
![]() |
mshiriki wa tamasha |
No comments:
Post a Comment