Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametoa amri ya kisheria ya kuanzishwa Mahakama ya Katiba nchini humo.
Taarifa kutoka Kinshasa zinasema kuwa, lengo la kuanzishwa mahakama hiyo, ni kudhamini taratibu za chaguzi za kitaifa nchini humo.
![]() |
| Rais wa kongo-Joseph Kabila |
Wakati huohuo, watu wawili wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya kutokea mapigano katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Kongo.
Viongozi wa kieneo wamesema kuwa, mapigano hayo yalitokea kati ya wanamgambo wa kundi la Raia Mutomboki na wale wa Mai Mai Nyatura.
Viongozi hao wameeleza kuwa, mapigano hayo yalianza baada ya wanamgambo wa Raia Mutomboki kuteketeza kwa moto vijiji vitatu, na kusonga mbele kuelekea mji wa Ngungu.
Naye Jean - Bosco Sebishimbo Mbunge wa Masisi, kwenye jimbo la Kivu Kaskazini amewataka viongozi wa kijeshi na kiraia nchini humo kuchukua hatua za haraka za kukomesha mapigano hayo.

No comments:
Post a Comment