
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa
Vyama vya Siasa.
Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na
kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa
uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.
Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa
Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa
mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano...
MSIMAMO WA RAIS KIKWETE KWA RAIS KAGAME WA RWANDA WAUNGWA MKONO KWA ASILIMIA 100 NA WASOMI HAPA NCHINI....

WASOMI na baadhi ya wanasiasa wazalendo nchini wameunga mkono
msimamo wa Tanzania uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kuhusiana na
chokochoko zinazoanzishwa na Rwanda na wamemtaka Rais wa nchi hiyo, Paul
Kagame, kukaa meza ya mazungumzo na waasi wa nchi hiyo walioko Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwani amani haiwezi kutafutwa kwa njia
ya mtutu wa bunduki.Akizungumza na MAJIRA kwa njia ya simu jana
Mhadhiri wa Chuo cha St. Agustino, katika kitivo cha sayansi ya siasa,
Prof. Mwesiga Baregu, alisema ushauri alioutoa Rais Kikwete kwa Rais
Kagame ni mzuri, hauwezi kuleta athari zozote tofauti...
No comments:
Post a Comment