UCHAGUZI wa Naibu meya katika Manispaa ya Shinyanga umefanyika jana
ikiwa Davidi Nkulila (CCM) diwani kata ya Ndembezi amerudia kuongoza
kiti hicho kwa kupata kura 14 zilizopigwa na wajumbe hao kati ya kura 22
huku mpinzani wake Nyangaki Shilungusheila (CHADEMA) diwani kata
ya Kambarage akiambulia kura nane
.
Katika uchaguzi huo ulioongozwa na mstahiki meya Gullamu Hafidhi
Mkadamu akiwepo na mkurugenzi wa manispaa hiyo Festo Kang’ombe
uliofanyika ndani ya ukumbi wa mkoa mara baada ya kumaliza kikao cha
bara za la madiwani huku zikiundwa kamati mbili za kudumu.
Hata hivyo kamati hizo ambazo ni kamati ya afya,elimu,uchumi na
fedha ambapo mwenyekiti wake Charles Njage ( CCM)diwani wa kata ya
Kizumbi alichaguliwa kwa kupigiwa kura na wajumbe waliokuwa ndani ya
kamati hiyo.
Aidha katika upande wa kamati ya miundombinu mwenyekiti alichaguliwa
Thomas Chuma (CCM) diwani wa kata ya Lubaga huku wajumbe wengine
wakiendelea kuchaguliwa kuwemo ndani ya kamati mbalimbali zilizopo.
Pia Nkulila aliwashukuru wajumbe kwa kumpatia kura za kurudi tena katika
uongozi kwa nafasi hiyo na kuwaahidi ushirikiana kama alivyokuwa
akifanya siku zote katika uongozi huo huku shilungushela akikubali
matokea hayo.
Alisema katika uongozi wake hapendelei mambo ya siasa katika vikao vya
kwenye baraza la madiwani bali kinachotakiwa ni kuwa kitu kimoja cha
kuwawakilisha wananchi matakwa yao walivyoyaagiza kuhusu siasa ni nje
mara baada ya kikao kumalizika.
Hata hivyo madiwani hao walipongeza uchaguzi huo ulikuwa wa uhuru na
haki, ikiwa mwanasheria wa manispaa hiyo James Mwakinya akisoma vifungu
vya kanuni na sheria vya uchaguzi huo kuwa uchaguzi huo ni wa
haki kwa kila mwaka kumpata naibu au makamu mwenyekiti ndani ya
manispaa.
No comments:
Post a Comment