EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, July 30, 2013

MIZENGO PINDA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KURUHUSU WANANCHI KUPIGWA

"WAPIGWE TU" YA MIZENGO PINDA ITAMFIKISHA KORTINI

KAULI ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ya kubariki vyombo vya dola kuendeleza kipigo kwa raia wanaokaidi amri imechukua sura mpya baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu (LHRC) kutangaza kumburuza mahakamani wiki hii kutokana na kushindwa kufuta kauli yake. Juni 20, mwaka huu, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni, Waziri Mkuu, Pinda, alivitaka vyombo vya dola kuendelea kuwapiga raia, akisema kuwa hakuna namna nyingine kwani serikali imechoka. Kauli hiyo imekuwa ikipingwa na wananchi, mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanasiasa wakimtaka Waziri Mkuu, Pinda, kuifuta kwa kuomba radhi, wakidai kuwa inachochea...

MBUNGE WA CCM ANAYEDAIWA KUFADHILI MADAWA YA KULEVYA AJISALIMISHA POLISI

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Iddi Azzan, aliyetajwa kwenye barua inayosadikiwa kuandikwa na wafungwa Wakitanzania waliopo Hong Kong “amejilisalimisha” kwenye ofisi za jeshi la polisi na kulitaka jeshi hilo lifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, ili hatua nyingine na ikibidi sheria, vichukue mkondo wake.Azzan amesema alienda mwenyewe kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam."Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainike  na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azzan...

KAHABA APEWA KICHAPO NA MALAYA WENZAKE KWA KOSA LA KUJIUZA KWA BEI YA HASARA NA MKOPO

  KAHABA  mmoja katika mji wa Naivasha, jimbo  la  Rift Valley  nchini Kenya amenusurika kufa baada ya kupewa kichapo kikali  na makahaba wenzake  wakimtuhumu   kujiuza  kwa  bei  ndogo  na  kuwaharibia  soko. Wenzake hao wenye hasira walimtwanga  kahaba  huyo  kwa ngumi   wakimshutumu kwa kutokuwa na ushirikiano na  kuwaharibia  soko hasa ikizingatiwa   kuwa  hivi  sasa  ni kipindi cha mwisho  wa mwezi  ambapo  mahitaji ya kununua ngono huoongezeka. Makahaba hao walitekeleza lengo hilo pale walipomzingira...

No comments:

Post a Comment