"WASANII WANAOVAA VIMINI KWENYE FILAMU HUWA WANAJIUZA"....MWAKIFAMBA
RAIS wa Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba amesema wasanii wanaovaa mavazi yasiyo na
staha ikiwemo vimini kwenye sinema wanajiuza.
Mwakifwamba aliyasema hayo katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga, jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, akiwa ameongozana na msanii Riyama
Ally.
Kauli hiyo ya Mwakifwamba imekuja siku chache baada ya sakata la uvaaji
vimini na udhalilishaji wanawake na wototo kwenye filamu kuzungumziwa bungeni,
Dodoma.
“Hili suala nimeshalikemea kwa muda mrefu sana... naamini kama ni watu wa
kuelewa watakuwa wameelewa na wale ambao wanaendelea na hayo mambo maana yake
ujue wana mambo yao.
“Siyo wote wanaoingia kwenye
filamu ni wasanii wa kweli, wengine wanatumia tasnia hii kutafuta mabwana ndiyo
maana wanavaa mavazi ya ajabu ili waonekane, jambo ambalo tunalikemea kila
wakati
"Sikatai wakati mwingine kuna ‘scene’ zitahitaji uhusika
fulani kama uchangudoa lakini utakuta msanii anatakiwa kuvaa uhusika wa
ofisini, yeye anavaa vinguo vya hovyo, maana yake ni nini kama si kutafuta
soko?” alisema Mwakifwamba na kuongeza:
“Imefika wakati wasanii wanatakiwa wabadilike kwani hali ilipofikia siyo
pazuri. Bado msanii anaweza kuonekana ana kiwango kizuri bila kuvaa nguo
zinazomdhalilisha na kumtafsiri vibaya mbele ya jamii.”
Akasema: “Sasa nasema hivi, yeyote atakayekiuka utaratibu tuliokubaliana
tutamchukulia hatua. Hatutamfumbia macho. Tunahitaji kuwa na tasnia yenye
heshima.”
RIYAMA SASA
Mkali wa kucheza na hisia, Riyama naye alitoa maoni yake kuhusu mavazi na
mwenendo mzima wa filamu za Kibongo ambapo kwa upande wake alisema anaamini
wanaofanya hivyo wanatafuta kuwa mastaa kwa njia ya mkato.
“Tatizo ni ulimbukeni wa kuiga wasanii wa nje. Wasanii tunakiwa kujitambua
na kufahamu na kulinda utamaduni wetu. Wasanii wengi hawajui thamani zao,
jamani ustaa siyo kukaa uchi.
“Tujue kuwa kwenye filamu siyo sehemu ya kutafutia mabwana. Kuonesha
urembo wetu wa nje na wa ndani kwenye hadhara siyo kitu kizuri kwa utamaduni
wetu... hao wanaofanya hivyo wanasababisha wasanii wote tuonekane machangudoa,”
alisema Riyama.
No comments:
Post a Comment