Hapo jana maafisa wa utawala nchini Afrika Kusini walisema kuwa Mandela alikuwa anaendelea vyema na matibabu baada ya kulazwa hospitalini kwa siku ya pili akiwa na maradhi ya kifua.
Taarifa kutoka rais wa nchi hiyo Jacob Zuma zilisema kuwa hali ya Mandela inaendelea kuimarika na kwamba hata aliweza kula vyema kiamsha kinywa chake.
Mapema leo Jacob Zuma, aliwahakikishia wananchi wa Afrika Kusini kuwa rais mstaafu Nelson Mandela anatibiwa ugonjwa wa mapafu ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara.
Katika mahojiano na BBC , bwana Zuma alisema kuwa watu hawapaswi kuwa na wasiwasi kwani Mandela anaendelea kupokea matibabu.
RAIS MANDERA -AFRICA KSINI
Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kabla ya Jumatano usiku.
Alikuwa hospitalini kwa siku 18 mnamo mwezi Disemba, akipokea matibabu ya mapafu na kibofu.
Katika taarifa yake iliyotolewa mapema, Zuma alisema kuwa Mandela anaendelea kupokea matibabu.
Rais Zuma hata hivyo hajaelezea alikolazwa Mandela.
Akiongea na mwandishi wa BBC Lerato Mbele, bwana Zuma alisema kuwa watu wanapaswa kuwa watulivu.
"ndio, nimekuwa nikiwambia watu kukubali kuwa Mandela sio kijana tena na ikiwa atakwenda hospitalini mwara kwa mara kwa ukaguzi wa kiafya, sidhani hilo linapaswa kuwaweka watu wasiwasi. Ningependa kusema kuwa watu hawapaswi kuwa na wasiwasi hata kidogo,'' alisema Zuma
Mandela anasifika na kujulikana kama Madiba jina la utani.
Alipohojiwa kuhusu ikiwa watu wa Afrika Kusini wajiandae kwa lolote , Zuma alijibu kusema kuwa ''ikiwa mzee anafariki, watu husema kuwa ameenda nyumbani.Nadhani hayo ndio baadhi ya mambo ambayo tunapaswa kutafakari.''
Lakini alisisitiza kuwa bwana Mandela ameweza kupokea matibabu vyema.
Bwana Mandela anatazamiwa na wengi kama baba wa taifa kwa kupambana dhidi ya enzi ya ubaguzi wa rangi.
Ni mara ya nne kwa Mandela kulazwa hospitalini katika muda wa miaka miwili.
Aliugua kifua kikuu mapema miaka ya themanini, alipofungwa jela katika kisiwa cha Robben Island, kwa miaka 18.
Mapafu yake inaarifiwa yaliathirika pakubwa kwa sababu ya kufanya kazi katika machimbo ya mawe alipokuwa anahudumia kifungo chake.
No comments:
Post a Comment