Luis Suarez anaamini kuwa atakua
tayari kwa mwanzo wa michuasno ya kombe la dunia baada ya kupata maumivu ya
goti na kufanyiwa upasuaji asubuhi ya siku nya jumatano yaani juzi.
Straiker huyo wa Liverpool na nchi
ya Uruguay alikwenda kufanyiwa uchunguzi na taarifa zilieleza kuwa suerez kwa
sasa anasaidiwa na kiti cha magurudumu kutembea ingawa mwenyewe amenukuliwa akisema.
"Nitakua safi na imara katika
siku chache zijazo na kwa asilimia 100 na nitaweza kuisaidia timu yangu ya
taifa katika michuano ya kombe la dunia”.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 27-
ameweka picha yake kwenye ukurasa wake wa twiter akiwa na familia yake, pamoja
na ujumbe unaosema: "Ahsante sana kwa jumbe za kuniunga mkono,upendo
pamoja na kunipa moyo ndani ya siku hizi za majeruhi!
"Ni nguvu ambayo wapendwa wangu
mnanipa/mnaionyesha kwangu... watanifanya nifanye kazi kwa bidiii na kufanikiwa
kushiriki kombe la dunia hii ni kwa familia yangu na watu wote mnaonisapoti!!"
Suarez alifanyiwa upasuaji baada ya
kutojisikia vizuri katika goti lake wakati wa mazoezi akiwa na timu yake ya
taifa ya Uruguay siku ya jumatano, na shirikisho la soka la Uruguay lilieleza
kuwa maumivu aliyoyapata suarez yanatokana na mshituko alioupata wakati wa
mechi za mwisho za michuano ya ligi kuu nchini uingereza dhidi ya Newcastle.
Timu ya taifa ya Uruguay itafungua
michuano ya kombe la dunia kwa kucheza na timu ya taifa ya Costa Rica tarehe 14 mwezi wa sita , na itafata mechi ya timu
taifa ya uingereza na italy.
Wakati huohuo mlinzi wa timu ya Newcastle
Paul Dummett, ambaye aliondolewa mara baada ya kumchezea rafu Suarez, amesema
kuwa amepokea jumbe za lawama toka kwa washabiki wa Uruguay kupitia ukurasa
wake wa twitter.
Akiongea na Mirror Dummett, amesema: "Ni changamoto ambayo
haiepukiki ni kweli alisababisha maumivu ya Suarez wakati walipokutana na
akajaribu kuchukua mpira kwa mguu wake wa kushoto ndipo akaanguka chini.
"lakini akasema kuwa anatuma
Suarez atashiriki michuano ya kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa kwani yeye ni moja ya wachezaji muhimu na
bora duniani hivyo anaamini atakua safi na atashiriki.
No comments:
Post a Comment