EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, March 22, 2014

MAKUBWA.......YANGA YAFANYIWA USHIRIKINA ILI WACHEZAJI WAKE WAKOSE PENALT UWANJANI

JINAMIZI la wachezaji wa Yanga kukosa penalti kisha kuandamwa limeonekana kuendelea ambapo sasa makubwa yamemkuta mshambuliaji wa timu hiyo, Hamis Kiiza baada ya kukosa penalti katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC, juzi. Kiiza, raia wa Uganda, alikosa penalti hiyo katika dakika ya 71 ambapo matokeo ya mwisho ya mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ni sare ya 1-1, hivyo Azam kuendelea kubaki kileleni ikiwa na pointi 44, huku Yanga ikishika nafasi ya pili kwa pointi 40.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Mara baada ya kipenga cha mwisho cha mchezo huo, mashabiki wengi wa Yanga walionekana kuchukizwa na kitendo cha timu yao kukosa ushindi, lakini zaidi ikiwa ni baada ya Kiiza kukosa penalti hiyo, ambapo walimvaa nahodha wao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kuanza kumlaumu kwa nini alikubali Kiiza apige penalti wakati wanaamini Cannavaro ni mzuri kwenye mikwaju hiyo.
Kabla ya kutoka uwanjani hapo, wachezaji wa Yanga walijifungia na kuanza kukosoana kutokana na kile kilichotokea kwenye mchezo huo ambacho kimesababisha Yanga kuwa na kazi ngumu ya kutetea ubingwa wake.
Penalti hiyo iliyotokana na beki wa Azam, Said Morad, kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, ilipanguliwa kiufundi na kipa chipukizi Aishi Manula.
Mara baada ya nusu saa kujifungia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo uwanjani hapo, tangu mchezo ulipomalizika, walitoka huku wakionyesha kuwa na hasira na kutoa lugha kali.
Hamis Kiiza.
Alipotoka Cannavaro mashabiki waliokuwepo eneo la karibu na lango la kutokea, wakamvaa na sehemu ya malalamiko yao yalikuwa hivi:
“Wewe ndiye mwenye timu yako, unaijua Yanga kitambo sana, siyo yeye (Kiiza), timu ikiharibika atarudi kwao Uganda kisha sisi ndiyo tutakaopata aibu hapa.
“Kwa nini hukupiga wewe ile penalti, sisi tuliona wewe unataka kupiga yeye amekuja kuchukua mpira na kuupiga, jambo hilo siyo zuri kabisa wala hatumfagilii, sisi tuna uchungu na timu hii kwani tunatoa pesa zetu.”
Cannavaro alikuwa akiwajibu mashabiki hao kwa sauti ya chini ambayo haikusikika kwa urahisi alichokuwa akikizungumza, alipoona umati unaongezeka, akaondoka na kuingia kwenye basi.
Kiiza alipotoka vyumbani humo, alionekana ni mwenye huzuni, mashabiki walianza kumtupia lawama, hakujibu kitu zaidi ya kuinama na kuanza kulia huku akielekea kwenye basi la wachezaji.
Akiizungumzia penalti hiyo, Aishi alisema ilikuwa ni ya kawaida: “Unajua sikuihofia kabisa ile penalti, kwani ilikuwa ni ya kawaida sana kwangu, nimekuwa nikizoea kudaka penalti tangu nilipokuwa katika timu B kwenye Michuano ya Uhai Cup.”

>>>grobal publishers

No comments:

Post a Comment