EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, June 18, 2013

HABARI KWA kina MSHIRIKI WA KIUME TOKA TANZANIA ( NANDO) YUKO HATARINI KUONDOLEWA BIG BROTHER



Ni wiki tatu zimepita tukishuhudia Eviction shows tatu zilizowapa tiketi za kurudi makwao washiriki 6 mpaka sasa, na tumeshuhudia mshiriki wetu Feza Kessy akiponea kwenye tundu la sindano baada ya kura za wa Tanzania na wa Afrika kumuokoa, sasa ni zamu ya Nando ambaye yuko hatarini wiki hii. Big Brother jana ametaja majina ya washiriki 7 ambao wako hatarini kutoka wiki hii na kati yao yupo kijana mpole, mtanashati, ‘handsome’ Nando anaeiwakilisha Tanzania, ikiwa ndio mara yake ya kwanza kupendekezwa . Washiriki wengine walipigiwa kura nyingi kutoka wiki hii ni love birds Bolt na Betty, ambao hii si mara yao ya kwanza kupendekezwa...
TUPE MAONI YAKO

KESI YA MENEJA WA MALAWI CARGO ANAYETUHUMIWA KUOMBA RUSHWA YA NGONO KWA MFANYAKAZI WAKE YAANZA KUUNGURUMA MAHAKAMANI


ALIYEKUWA  Meneja wa Kampuni ya Malawi Cargo tawi la Mbeya Evason Mwale(49) raia wa nchi jirani ya Malawi, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya akituhumiwa kujihusisha na Rushwa ya Ngono. Mwendesha mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe akisoma Mashtaka ya mtuhumiwa huyo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuluo alisema Mtuhumiwa anashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni Rushwa ya Ngono kinyume cha kifungu cha 25 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2007. Namkambe alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa anashtakiwa kwa kosa lingine la matumizi mabaya ya...
TUPE MAONI YAKO

BAADA YA NAPE KUITUHUMU CHADEMA, MBOWE NAYE AFUNGUKA NA KUDAI KUWA BOMU LILIRUSHWA NA FFU NA USHAHIDI ANAO


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefichua siri kuhusu tukio la mlipuko wa bomu lililotokea jusi katika viwanja vya Soweto, jijini Arusha.Katika kauli yake jana, Mbowe ameibua tuhuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi, ambapo alidai kuwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) ndiye aliyerusha bomu hilo.Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,baada ya kutembelea majeruhi katika Hospitali ya Selian, Mbowe alisema chama chake kina ushahidi wa kutosha juu ya askari huyo kurusha bomu.Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,alisema wamefanikiwa kupata ushahidi wa kutosha juu...
TUPE MAONI YAKO

CATHY WA BONGO MOVIE ALIA NA USHIRIKINA ULIPO NDANI YA TASNIA HIYO....AWATAKA WASANII WAMRUDIE MUNGU


Mwigizaji wa Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’  naye amenyanyua kinywa chake na kuonesha jinsi gani anakerwa na wasanii wanaoshinda kwa waganga ili kutafuta ustaa. Akiongea na mwandishi  wetu hivi karibuni, Cathy alisema kuna baadhi ya wasanii (hakuwataja majina) wamekuwa na tabia za kuzunguka kwa waganga wakitafuta kuwa juu katika tasnia ya filamu suala ambalo halipendezi na kuwasihi wawe na hofu ya Mungu. “Vifo vya wasanii vimetokea vingi sana, nilidhani kutokana na vifo hivyo wangepata hofu ya Mungu na kuacha mambo yasiyofaa vikiwemo vitendo vya kishirikina lakini hawakomi, wananikera sana. Ipo siku wataumbuka kwani...
TUPE MAONI YAKO

KAULI YA SERIKALI KUHUSU KITITA CHA MILIONI 100 KWA MTU ATAKAYEMTAJA MTU ALIYERUSHA BOMU ARUSHA


Zifuatazo ni nukuu za maneno yaliyotolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, sera, uratibu na bunge William Lukuvi kuhusu hilo bomu ambalo lililipuliwa kwenye mkutano cha Chadema Arusha. “Mtu asiejulikana alirusha kitu katika kundi la watu kilichosababisha mlipuko mkubwa, mkutano huu ulikua na ulinzi wa jeshi la Polisi wakiwa na magari mawili… askari walisimama upande wa Kaskazini ya uwanja ambapo mrushaji alikua mashariki na alirusha bomu kuelekea Magharibi” “Jaribio la Askari Polisi kutaka kumfata alierusha lilizuiwa na makundi ya Wananchi ambao walianza kuwashambulia polisi kwa mawe na kuwazomea na hivyo Polisi kulazimika...
TUPE MAONI YAKO

MSHIRIKI WA TANZANIA ( FEZA KESSY ) AKIMUOGESHA MSHIRIKI WA ZIMBABWE ( HAKEEM) NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER


Video hizi  hutolewa na big borther wenyewe kwa jamii kama sehemu ya shindano hilo.... Wahiriki wote wa big brother wanajua  ya  kwamba jumba hilo limezingirwa na kamera kila kona.Kwa hiyo, kama mtu ataamua kufanya ufuska au kukaa uchi basi ajue kamera zitamrekodi na kumwanika hadharani.... Masharti hayo hujuzwa mapema kabla ya kuanza kwa shindano hilo... Hakeem Huyu ni mshiriki toka zimbabwe aliyepata bahati ya kuoga na dada yetu Feza ndani ya bafu moja  Feza  Huyu ni mshiriki toka Tanzania....Yuko ndani ya afu moja akioga na mshiriki  wa Zimbabwe..... Dakika chache baada ya kila mmoja kuoga...
TUPE MAONI YAKO

VIDEO YA NAPE NNAYE AKIWAVAA CHADEMA NA KUDAI KUWA WANAHUSIKA NA MLIPUKO WA BOMU


Wakati jeshi la polisi na vyombo mbalimbali vya usalama vikihaha kumtafuta mtu aliyerusha bomu katika mkutano wa kampeni huko Arusha chama cha mapinduzi CCM kimetoa tamko kuhusiana na tukio hilo na kukishutumu moja kwa moja chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kuwa wao ndio wanaohusika na tukio hilo .   ...
TUPE MAONI YAKO

VIDEO MBILI ZA MAZISHI YA MSANII LANGA KILEO

Hizi ni video zinazoonesha shughuli nzima ya kuuaga mwili wa Langa Kileo na baadaye kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Wakati wa kuuaga mwili ...
TUPE MAONI YAKO

VIDEO YA MLIPUKO WA BOMU LA TAREHE 15 HUKO ARUSHA


Hii ni video fupi ambayo nimepata katika mtandao wa youtube ikionesha jinsi bomu hilo lilivyolipuka na wananchi kutawanyika...
TUPE MAONI YAKO


"MLIPUKO WA BOMU LA ARUSHA ULIPANGWA NA CHADEMA WENYEWE".....NAPE NNAUYE


Itakumbukwa tarehe 16/06/2013 ilikuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa madiwani kwa baadhi ya kata nchini. Uchaguzi huo umefanyika kwenye kata ishirini na mbili (22) -kati ya kata ishirini na sita (26) zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi. Matokeo tuliyoyapata toka kwenye maeneo yaliyofanya uchaguzi yanaonyesha kuwa kati ya kata 22 zilizofanya uchaguzi CCM tumeshinda kata 16 sawa na asilimia 72.72% na wenzetu wamechukua kata 6 zilizobaki sawa na asilimia 27.28%. Tunawashukuru sana kote walikoonyesha imani yao kubwa kwa Chama chetu kwa kutupa dhamana ya kuendelea kuwatumikia. CCM inawaahidi utumishi uliotukuka.  Hata...
TUPE MAONI YAKO



...

No comments:

Post a Comment