EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014
Showing posts with label TOA MAONI YAKO JUU YA HIKI. Show all posts
Showing posts with label TOA MAONI YAKO JUU YA HIKI. Show all posts

Friday, May 23, 2014

JEURI YA PESA HIYO!, PSG WATAKA KUMSAJILI DAVID LUIZ KWA DAU LA PAUNDI MILIONI 50 NA KUVUNJA REKODI YA DUNIA

Pointing to the sky: Chelsea star Luiz is on the brink of joining PSG in a deal costing close to £50 millionNyota wa Chelsea,  Luiz yuko njia kuelekea PSG kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 50.
NDANI ya saa 48 zajazo, David Luiz anaweza kujiunga na Paris St Germain kwa dau nono la paundi milioni 50.
 Kiwango halisi cha ada ya uhamisho kitatajwa na klabu, lakini uhamisho wa beki huyo wa Chelsea mwenye miaka 27 utavunja rekodi ya dunia kwa uhamisho wa mabeki.
PSG iliweka rekodi ya kuwasajili mabeki wawili Marquinhos na Thiago Silva kwa dau nono zaidi, lakini kama watamnasa Luiz kwa mkwanja huo watavunja rekodi hiyo.
Kama dau hilo litakubaliwa  Stamford Bridge, PSG wataomba ruhusa kwa kocha wa Brazili Luiz Felipe Scolari ili wakamchukua vipimo vya afya wakati huu anapojiandaa na kombe la dunia.
Tongue out: Luiz celebrates with the Europa League trophy after Chelsea beat Benfica in the 2013 finalPSG  wanaamini kumsajili Luiz watakuwa wamefanikiwa kusajili beki bora zaidi duniani na usiku wa jana walionekana kuwa tayari kulipa kiwango chochote watakachohitaji Chelsea.
Matajiri hao wa Ufaransa wanataka kuonesha umwamba wao wa kifedha kwa mara nyingine tena majira ya kiangazi. 
Vyanzo vya habari mjini Paris vimethibitisha kuwa PSG wanajipanga mapema kuwapiga bao Barcelona na Bayern Munich wenye nia ya kumsajili.
Na inaaminika kuwa kwa dau hilo PSG hawana mpinzani. 
Chelsea watatumia fedha hizo kuimarisha kikosi chao kwa kumchukua nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa.

Sunday, January 19, 2014

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MKE WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mheshimiwa Damian Zefrin Lubuva kufuatia kifo cha Mke wake, Mama Martha Peter Lubuva kilichotokea tarehe 17 Januari, 2014 katika Hospitali ya Apollo iliyoko New Delhi nchini India alikopelekwa kwa matibabu akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Mke wako, Mama Martha Peter Lubuva aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Apollo nchini India akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Kisukari ambao umesumbua kwa muda mrefu”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake za Rambirambi.
Rais Kikwete amesema anatambua fika machungu ambayo hivi sasa wanapitia watoto na Familia nzima ya Mheshimiwa Damian Zefrin Lubuva kutokana na kuondokewa na Mama yao Mzazi na Kiongozi
muhimu wa Familia, lakini amewaomba wawe watulivu na wavumilivu, lakini muhimu zaidi wawe na moyo wa ujasiri katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao.
“Ninawahakikishia kuwa niko pamoja nayi katika kuomboleza msiba huu mkubwa na namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Mama Martha Peter Lubuva kwa kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake Mola”.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
DAR ES SALAAM.
18 Januari, 2014

Viongozi wa kisiasa waonywa kuitumia TAHLISO

MWENYEKITI mstaafu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taaluma za Juu Tanzania (TAHLISO), Amon ChakushemeireMWENYEKITI mstaafu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taaluma za Juu Tanzania (TAHLISO), Amon Chakushemeire, amesema jumuiya hiyo inaendeshwa kitaaluma na si kisiasa.
Chakushemeire aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi nafasi hiyo kwa mwenyekiti mpya wa TAHLISO, Moses Mdee, na kueleza kuwa viongozi wa kisiasa wanapaswa kuacha kuitumia jumuiya hiyo kwa lengo la kujinufaisha.
Alisema kuwa wapo baadhi ya wanasiasa wanaotaka kuwania nafasi za juu za uongozi wamekuwa wakiingilia majukumu ya kiuongozi ya jumuiya hiyo.
“Wapo wanasiasa wanaotarajia kugombea urais mwaka 2015 wanaingilia uongozi wa TAHLISO kwa utashi wao ili iendeshwe kisiasa, hali iliyosababisha kutaka kuingiza usiasa na kutuletea wagombea wao katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana,” alisema.
Chakushemeire alisema licha ya jumuiya hiyo kutegemea taasisi za nje katika kujiendesha, lakini katiba yao hairuhusu kushirikishwa wanasiasa ikiwemo kusaidiwa na taasisi zinazojiendesha kisiasa.
Alisema changamoto inayoikabili TAHLISO ni wimbi la wanafunzi wa elimu ya juu kugubikwa na siasa badala ya kuweka malengo katika elimu itakayowanufaisha kwa maisha yao ya baaadae.
“Ni jambo la kusikitisha kuona elimu yetu sasa ni uwanja wa siasa, wanasiasa wengi wanawatumia wanafunzi wa elimu ya juu kujinufaisha kisiasa ikiwa ni pamoja na kupiga kampeni za siri siri,” alisema.
SOURCE: TANZANIA DAIMA

NAPE AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA MAGOMENI BAGAMOYO

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Bagamoyo alipowasili kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za udiwani kata ya Magomeni.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa shina la wakereketwa la stendi ya Kangowe mara baada ya kulifungua shina hilo.
 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga ngoma ya asili ya watu wa Bagamoyo kabla ya kuanza kuhutubia wakazi wa kata ya Magomeni.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo kwenye viwanja vya shule ya msingi Majengo na kuwataka wananchi wa kata hiyo kufanya maamuzi sahihi kwa wakati huu kwa kumchagua mgombea kutoka CCM kwani ndio chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa.

 
 Wapenzi na Wanachama wa  Chama Cha Mapinduzi wakijumuika kucheza ngoma ya asili ya Bagamoyo.


 
 Mgombea wa Kiti cha Udiwani Kupitia CCM Mwanaharusi Hamis Jarufu akipiga magoti kwa wapiga kura wake kama ishara ya kuomba kura.
 Mgombea wa Kiticha Udiwani kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo kwa tiketi ya CCM Mwanaharusi Hamisi Jarufu akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni wakati wa uzinduzi wa kmapeni za udiwani wa kata hiyo.

TBS kuwasaka waingizaji wa nguo za ndani


Mitumba nguo za ndaniSHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) litafanya operesheni ya kuwasaka wale wote wanaoingiza nguo za ndani za mitumba nchini.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili jana, Ofisa Mahusiano wa TBS, Roida Andusamile, alisema kuwa hivi sasa wameanza kuwakamata wafanyabiashara wadodo wadogo katika masoko mbalimbali ya jijini Dar es Salaam ili kubaini zinapotoka nguo hizo.
Alisema kuwa nguo hizo zimepigwa marufuku kutokana na kuwa na athari za kiafya hivyo hazihitajiki kuingizwa sokoni.
Andusamile alizitaja nguo ambazo zimepigwa marufuku ni pamoja na soksi, nguo za ndani kwa wanawake na wanaume, pamoja sidiria.
“Kufanya biashara hii ni kosa kubwa kwa kuwa zinahatarisha maisha ya Watanzania ambao hawana hatia, pia sheria iko wazi ambayo ilipitishwa mwaka 2003 ikipiga marufuku uingizaji wa nguo hizi,” alisema.
Alisema kuwa katika msako wa wafanyabiashara ndogo ndogo walikamata nguo hizo katika manispaa zote za jijini na kulazimika kuziteketeza.
Alisema kuwa kuwa endapo wakikamata mfanyabiashara mdogo asipotoa ushirikiano anakozipata nguo hizo atalazimika kulipa faini ya sh milioni 50 hadi 100.
SOURCE: TANZANIA DAIMA

SIKILIZA WAHANGA WA MAAFA YA MVUA NANYAMBA MKOANI MTWARA WAKIELEZEA JINSI ILIVYOKUWA MBELE YA MKUU WA WILAYA PAMOJA NA KILE SERIKALI ILICHOSEMA JUU YA WAHANGA HAO