Wilaya ya Mkuranga inakabiliwa na tatizo kubwa la ukataji miti hiyo kwa ajili ya kutengeneza mkaa ambao uma soko kubwa mkoani Dar es Salaam .
Hayo alisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mkuranga, Saada Mwaluka wakati akifunga mafunzo ya utengenezaji wa mkaa na kuni mbadala mjini hapa.
Alisema soko kubwa la mkaa lipo mkoani Dar es Salaam kwa kutegemea miti inayokatwa kwa wingi wilayani Mkuranga hali ambayo inasababisha kutokea kwa uharibifu wa mazingira na jangwa.
Alisema misitu wilayani humo ipo hatarini kutoweka, hivyo ili kunusuru hali hiyo wameanzisha mpango wa kuhamasisha wananchi na kuwapatia mafunzo ili wajue umuhimu wa utunzaji mazingira pamoja na misitu.
Mwaluka alisema mafunzo ya teknolojia ya utengenezaji wa mkaa bora na uandaaji wa mpango biashara itakuwa chachu ya uhamasishaji wa matumizi bora na sahihi ya nishati za tungamotaka katika maeneo hayo.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment