Kutoka
kushoto ni Miss Tanzania 2013 Happy Watimanywa , Dk. Agnes Nyomola
kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye ni Mtaalam wa mambo ya
Sayansi, na Specioza Rweyemamu ambaye ni Ispecta katika mambo ya anga
katika Mamlaka wa usafiri wa Anga Tanzania, ambao ndio walikuwa wasemaji
katika sherehe hizo
Dk.
Agnes Nyomola kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye ni Mtaalam wa
mambo ya Sayansi akizungumza na wanafunzi kutoka shule mbalimbali jijini
Dar es salaam waliofika katika sherehe hizo za siku ya wanawake Duniani
na kuwasihi kupenda masomo ya Sayansi kutokana na kwamba kwa sasa Dunia
imebadilika na tunapo elekea ni Karne ya Sayansi na Teknolojia,
amewasihi pia wasichana kupenda masomo hayo akiamini kuwa wanaweza na
kwamba ni Fursa muhimu sana kwao.
Specioza
Rweyemamu ambaye ni Ispecta katika mambo ya anga katika Mamlaka wa
usafiri wa Anga Tanzania akizungumza na wanafunzi pamoja na wageni
waalikwa mbalimbali hasa wanafunzi na kuwaasa kuwa wanatakiwa kuwa mfano
wa kuigwa katika jamii na kusoma kwa bidii kwani hakuna kisicho
wezekana kila mtu anaweza, pia amewasihi wasichana hasa wadogo kupenda
kusoma zaidi ili waje kuwa viongozi wa baadae.

Wakili
wa Mahakama Kuu Modesta Mahiga akizungumza na wanafunzi waliofika
katika Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Chuo Kikuu Dar es salaam na
kuwahimiza wanafunzi hasa wakike wanaokuwa wasikimbilie katika mambo
makubwa lakini wakazane na masomo ili kupata kufanikiwa zaidi.

Miss
Tanzania 2013 Happy Watimanywa akiongea na wanafunzi, alisisitiza sana
wanafunzi wenzake wa kike kuwa wanatakiwa kusoma kwa Bidii ili kuweza
kuja kufanikiwa katika mambo yao ya mbeleni, aliongeza kuwa mtoto wa
kike ndio taifa la kesho na kiongozi wa kesho hivyo ni lazima wakazane
sana katika masomo yao na kuichukulia siku ya leo kama changamoto na
chachu kwao ya kujibidisha zaidi.

Mwenyekiti
wa Muunganiko wa mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotetea haki za
Wanawake Tanzania Bi. Juliana Bwire akitoa neno la Shukurani kwa
wasemaji wote waliokuwa wakizungumza kila mmoja kwa wakati wake , pia
kuwashukuru wote waliofika katika Sikukuu hiyo ya Mwanamke Duniani.
Jane Mrema Mshauri wa
Jinsia kutoka Shirika la Plan International akielezea nia yao kubwa ya
kushiriki katika Sherehe hizo leo.

<![endif]-->Gloria
Chambo mwanachama wa chama cha Muunganiko wa mashirika yasiyo ya
Kiserikali ambaye ndiye alikuwa mshereheshaji wa Siku hiyo ya wanawake
akizungumza Jambo wakati wa Sherehe hizo na kuongoza ratiba hiyo.

Baadhi ya wanafunzi wa
shule mbalimbali kutoka Jijini Dar es salaam wakiwa wanafuatilia mambo
mbalimbali yanayo endelea wakati wa sherehe hizo.

Hawa ni wanafunzi wa
Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu walemavu wa jumla, wakiwa
wanafuatilia kwa umakini kinacho endelea uwanjani hapo.

Msichana mfupi Mbele ni
Mwanafunzi wa Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Jovina Vedastus
ambaye ni Fundi wa Ushonaji na utengenezaji wa Batiki akicheza muziki
ambapo alikonga nyoyo za watu wengi kwa umahili wake huo katika kucheza.

wanafunzi wa Chuo cha
ufundi kwa watu wenye ulemavu walemavu wa jumla, hapa wakiwa viziwi,
wasio ona, wenye ulemavu wa Miguu , mikono mapoja na Matatizo mengine
wakiwa wanatumbuiza na burudani ya aina yake ambapo watu wengi
walivutiwa sana na kufurahishwa.

Mwakilishi kutoka OXFAM
ambao pia ni wanachama wa chama cha Muunganiko wa mashirika yasiyo ya
Kiserikali Afisa utetezi wa haki za kiuchumi OXFAM Bi.Mkamiti Mgawe
akifunga Rasmi sherehe hizo na kuwashukuru wote waliofika katika katika
sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es
Salaam leo.

Hili lilikuwa ni Tukio
la Aina yake ambapo Miss Tanzania 2013 Happy Watimanywa alipo vamiwa na
wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari Jijini Dar es salaam
wakiomba awasainie katika Madaftari yao kama kumbukumbu ya kwamba na wao
walisha wahi kumuona Mrembo huyo, Hapa akiwa anasaini katika Baadhi ya
Madaftari hayo.
No comments:
Post a Comment