EBENEZA MARCH 9 2014
SWACO
royal
tt
NIMO
mvuto
Wednesday, January 22, 2014
DC WA WILAYA YA NANYUMBU ATOA ONYO KALI KWA WANASIASA WANAOSHAWISHI WAKULIMA KUGOMA KUKATWA FEDHA ZA MAENDELEO NA PEMBEJEO.
Na Mohamed Mwaya
MKUU wa Wilaya ya Nanyumbu, Mkoa wa Mtwara, Festo Kiswaga
amesikitishwa na harakati zinazofanywa na wanasiasa kuchochea migomo
na maandamano katika awamu ya pili ya malipo ya korosho kukatwa fedha
shilingi 60 za pembejeo na maendeleo na kuahidi kuwachukulia hatua
kali.Kauli hiyo alitoa jana katika kikao kilichofanyika ofisini kwake
pamoja na viongozi wa vyama vya msingi vilivyopo wilayani humo na
kusisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa wanasiasa wote
watakaobainika kuhusika na migomo hiyo.
Kiswaga alisema kuwa vyama vyote vya msingi lazima vichangishe fedha
hizo kwa ajili ya maendeleo ya wilaya pamoja na kuwatunzia fedha za
pembejeo wakulima wa korosho wakati waaanza kuandaa mashamba wapate
pembejeo zao bila usumbufu.
“Tunachokiangalia sasa ni kuona jinsi gani tunapiga hatua kuelekea
mafanikio makubwa natoa agizo kwenu wanasiasa wote nitakaowabaini
kuhusika na migomo na kuchochea fujo kwa wakulima kugomea kukatwa
shilling 60 kwa kilo hatua kali lazima zichukuliwe,”alisema Kiswaga.
Katika kukazia hilo alisema kuwa hadi kufika Januari 30 mwaka huu
vyama ambavyo havijatekeleza agizo hilo viongozi watachukuliwa hatua
pamoja na kuwang’oa madarakani kwani wankwamisha maendeleo ya wananchi
pamoja na kuzorotesha uchumi wa wilaya hiyo.
“Nasema kuwa kama ukitaka kuwa adui na mimi usiende kuchangisha fedha
hizo za pembejeo shilingi 30 na maendeleo shilingi 30 kwa kila kilo
kwani utakuwa mpinga maendeleo,”alisema.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya aliwaonya viongozi kuacha
tabia za kusafirisha fedha za vyama vya msingi kwa njia ya pikipiki
kitendo ambacho kinachangia ongezeko la wizi na kukwamisha na kuweka
madeni makubwa ndani ya vyama hivyo.
Pia aliwakumbusha kuwa viongozi hao watenganishe siasa na uongozi wa
vyama vya msingi kwani kwani wao wakiyumba basi maendeleo nayo
yatayumba na kusababisha uchumi wa wananchi kukwama.
Naye mwenyekiti wa chama cha msingi cha Msweno AMCOS Fatuma Chisanga
alisema kuwa vyama vya msingi ndivyo vinavyochangia maendeleo ya
wilaya hiyo kuliko sekta nyingine zote.
Msimu wa mwaka 2013 wilaya hiyo ilikusanya na kuuza tani 6000 tu
ambapo mkuu wa wilaya hiyo anataka kuweka mikakati ya kufufua na
kuendeleza mikorosho ili msimu wa mwaka 2014 upande hadi kufikia tani
10,000.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment