EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, November 28, 2013

ZLATAN: SIHITAJI BALLON d'OR, NAJUA MIMI NI BORA."

Zlatan Ibrahimovic: Cristiano Ronaldo can have the Ballon d'Or, I already know that I am the best
IBRAMOVIC CADABRA
 
Mshambuliaji huyo wa Sweden amekuwa kwenye fomu nzuri sana msimu huu na klabu yake ya Paris St Germain, akifunga mabao nane katika Champions League - sawa na Cristiano Ronaldo.

Ronaldo anaonekana kupewa nafasi kubwa kushinda tuzo hiyo ya  Fifa-Ballon d'Or baada ya hat trick yake katika ushindi wa Ureno dhidi ya Sweden wiki iliyopita na hivyo kuiwezesha nchi yake kufuzu kushiriki michuano ijao ya kombe la  dunia. 

Winga wa Ufaransa Ribery aliisaidia Bayern Munich kushinda makombe matatu msimu uliopita na alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kutwaa mwanzoni. 
 
"Sihitaji Ballon d'Or kujua kwamba mimi ni bora," alisema Ibrahimovic, ambaye pia amesaidia timu yake ya PSG  kuvuka hatua ya makundi. 
"Hii tuzo ina maana kubwa kwa wachezaji wengine."
 
Hakuna msweden aliywahi kushinda Ballon d'Or au mchezaji bora wa mwaka wa FIFA lakini hilo jambo halimkoseshi usingizi hata kidogo Cadabra.
 
"Sio kitu ambacho nakifikiria sana na sio kitu ambacho kina umuhimu kwangu," alisema.
 
Hatahivyo mshambuliaji huyu amejiandikia historia nyingine ya kuingia katika list ya wachezaji waliofikisha michezo 100 katika michuano klabu bingwa ulaya 
 
 

No comments:

Post a Comment