EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, November 7, 2013

ASHLEY YOUNG ATISHIA WAINGEREZA KWA TABIA YAKE YA KUJIRUSHA UWANJANI AKIDAI PENALT



MWINGEREZA Ashley Young Alipoanguka Na Kuisaidia Manchester United Kupata Penalti Kwenye Mechi Ya Ligi Ya Mabingwa Ulaya Dhidi Ya Real Sociedad Usiku Wa Juzi Jumanne, Hakuna Aliyeshangazwa.


Staa Huyo Ana Historia Ya Kujiangusha Na Alishawahi Kukanywa Na Kocha Wake Wa Sasa David Moyes Na Hata Yule Wa Zamani Sir Alex Ferguson Kuhusiana Na Tabia Hiyo Mbaya Mchezoni. Kitendo Cha Kujiangusha Mara Kwa Mara Kinawakera Wengi,  Wanachukizwa Na Young Kwasababu Amekuwa Akiwadanganya Waamuzi Na Kutoa Penalti Ambazo Kiuhalisia Hazina Ukweli Wowote.
Kwenye Ligi Kuu England, Young Amesababisha Penalti Zaidi Ya Nne Ambazo Zinatokana Na Kujiangusha Kwake, Kwenye Timu Ya Taifa Amesababisha Penalti Moja.
Penalti Yake Katika Mechi Na Sociedad Imewachefua Wengi Na Kuanza Kuorodhesha Idadi Ya Penalti Zote Zenye Utata Ilizopata Manchester United Na England Zilizosababishwa Na Winga Huyo Wa Zamani Wa Aston Villa.




Novemba 5, 2013: Man United 0-0 Real Sociedad
Sawa Haukuwa Usiku Mzuri Kwa Robin Van Persie Na Javier Hernandez Baada Ya Kuikosesha Manchester United Ushindi, Huku Marouane Fellaini Naye Akishuhudia Kadi Nyekundu. Lakini, Aliyetibua Zaidi Usiku Huo Mtamu Wa Ligi Ya Mabingwa Ni Winga Ashley Young, Ambaye Aliendelea Na Utamaduni Wake Wa Kujiangusha Na Kutengeneza Penalti.
Baada Ya Kuwadanganya Marefa Wengi England, Safari Hii Young Aliweza Kumrubuni Mwamuzi Mtaliano Nicola Rizzoli Mbele Ya Mashabiki Wapatao 28,000 Kwa Kujiangusha Na Kusababisha Penalti Kwa Manchester United.
Young Alikwenda Chini Kirahisi Sana Baada Ya Kupokea Pasi Ya Kisigino Kutoka Kwa Shinji Kagawa, Lakini Kilichowakera Wengi Ni Jinsi Alivyojiangusha Utadhani Amefanyiwa Faulo Kubwa. Hata Hivyo, Manchester United Ilishindwa Kufunga Mkwaju Huo Wa Penalti Baada Ya Mdachi Van Persie Kukosa.
Septemba 14, 2013: Man United 2-0 Crystal Palace
Kwenye Mchezo Huu, Young Alishitukiwa Na Mwamuzi Jon Moss Na Kuonyeshwa Kadi Ya Njano Kutokana Na Kujiangusha Baada Ya Kuguswa Na Kagisho Dikgacoi. Lakini, Kwenye Mchezo Huo Huo, Baadaye Alijilegeza Tena Na Kwenda Chini Kirahisi Na Kusababisha Penalti Huku Akimsababishia Dikgacoi Kutolewa Kwa Kadi Nyekundu.
Baada Ya Tukio Hilo, Moyes Alisema: “Sitaki Wachezaji Wangu Wajiangushe. Nitamweleza Ashley Kitu Kama Kile Sitaki Kukiona.” Kwa Tukio La Mechi Na Sociedad Inaonekana Ni Ngumu Kwa Staa Huyo Kuacha Tabia Yake Hiyo Mbaya Ya Kuuchafua Mchezo Mzuri Wa Soka.

No comments:

Post a Comment