Serikali imewataka waganga wa tiba asili hapa nchini, washirikiane na wataalamu wa utafiti, ili kuwezesha upatikanaji wa dawa bora na salama.
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii,
![]() |
Waziri wa Afya-dR: hUSSEIN Mwinyi |
Dk.Hussein Mwinyi ametoa kauli hiyo wakati akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya siku ya tiba ya asili ya mwafrika, ambayo huadhimishwa kila mwaka Agosti 31, lakini mwaka huu hayakufanyika kutokana na uhaba wa fedha. Dk.Mwinyi amewataka waganga hao kushirikiana na watafiti kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Taasisi ya Utafiti wa Dawa za Asili iliyokpo katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shiriki- (MUHAS).
Ameongeza kuwa waganga wote wa tiba asili na tiba ya kisasa, wanatakiwa kufanya kazi kwa kuelewana, ili kuwezesha kupata taarifa za awali kabla ya utafiti kamili kufanyika.
Ameitaja kauli mbiu ya maadhimisho hayo kuwa ni ' Tiba Asili : Utafiti na Maendeleo' kuwa inalenga kutoa majukumu kwa waganaga wa tiba asili na tiba mbadala katika sula zima la utafiti.
No comments:
Post a Comment