EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, October 22, 2013

MUNUSCO YASHANGAZWA NA KONGO KUWACHEKEA WANAOKIUKA HAKI ZA BINADAM



Tume ya umoja wa mataifa nchini jamhuri ya kidemokrasia ya kongo monusco, imesema inasikitishwa na kutokuwepo kwa maendeleo katika juhudi za kuwafikisha kwenye mikono ya sheria, watu wanaohusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu katika jimbo la kivu kusini.
Monusco imesema hadi sasa watu waliohusika na ukiukaji wa haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya ubinadamu, ikiwa ni pamoja na wanajeshi wa jeshi la serikali ya drc waliohusika na makosa ya ubakaji yaliyotokea mwezi novemba mwaka jana mjini minova, kivu kusini hawajifikishwa mahakamani. Mwakilishi wa umoja wa mataifa nchini drc martin kobler amesema serikali ya drc inatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za kimataifa na sheria za drc.
Mwezi april mwaka jana wanawake 103 na wasichana 33, wengine wakiwa na umri wa miaka sita, walibakwa na wanajeshi wa jeshi ya la serikali ya drc, wakati wakiyakimbia majeshi ya kundi la m23.

No comments:

Post a Comment