| MKUU WA WILAYA MTWARA MH: WILLIMAN KAPENJAMA NDILE.........PICHA NA MAKTABA |
MKUU Wa Wilaya Ya Mtwara
MH: Williman Kapenjama Ndile Ametangaza Siku Saba Kwa Wazazi Kupeleka Watoto
Wote Waliofaulu Kujiunga Na Shule Za Sekondari Katika Wilaya Yake Kwenda Kuanza
Muhula Wa Masomo Kabla Ya Hatua Za Kisheria Kuanza Kuchukuliwa Kwa Wazazi
Watakaobainika Kutopeleka Watoto Hao Shuleni.Akizungumza Mapema Leo Asubuhi Kupitia
Kipindi Cha Radio Cha Amka Na Pride Kinachorushwa Na Kituo Hiki Mh: Ndile Alisema
Kuwa Mpaka Sasa Wilaya Bado Iko Nyuma Kielim Na Kwamba Kwa Mwaka 2014 Wanafunzi
Wote Waliofaulu Mtihani Wa Darasa La Saba Ni Wanafunzi Watatu Tu Ndio
Waliojiunga Na Kidato Cha Kwanza Kati Ya Wanafunzi Kumi Ya Hao.
Wakati Akitoa
Maelezo Hayo Mkuu Huyo Pia Ametangaza Rasmi Siku Saba Za Kisheria Kwa Wazazi
Kupeleka Watoto Walioko Mitaani Katika Shule Zao Walizofaulu Na Kwamba
Wasipofanya Hivyo Mpaka Kufikia Jumatatu Ijayo Ya Tarehe 24 Wote Watafikishwa
Mahakamani Kujibu Mashitaka Ya Kwa Nini Hawataki Kuwapeleka Watoto Wao Shuleni.
Aidha Katika Kutilia
Mkazo Swala Hilo Mh: Ndile Amesema Kuwa Tayari Amekwishawaandikia Barua Za Amri
Ya Kamatakamata Hiyo Watendaji Wote Na Maafisa Tarafa Wa Wilaya Yake Pamoja Na OCD
Na Kwamba Jumatano Ya Wiki Hii Kutakuwa Na Kikao Kikubwa Cha Pamoja Kati Ya
Ofisi Yake Na Maafisa Tarafa,Watendaji Na Polisi Wa Ngazi Ya Kata Kuzungumzia
Juu Ya Hatua Alizozipanga.Mwisho Aliwataka Wanamtwara Kubadili Mawazo Ya Kuwa
Elimu Ni Gharama Na Kwamba Lazima Waangalie Mazingira Yaliyopo Sasa Bila Ya
Elimu Hakuna Kinachowezekana Na Kutoa Rai Kuwa Hata Kama Mtwara Fursa Zikaja Za
Kutosha Kama Watu Wasipokuwa Na Sifa Ya Elimu Bado Wenyeji Watabaki Bila Kazi
Na Kushindwa Kuzitumia Fursa Zilizopo Mkoani Na Ndani Ya Wilaya Zao.
| MH:...NDILE |
Alisema Pia Hata
Unapozungumzia Miaka Mitano Ijayo Mtwara Itakua Ndio Mji Unaoongoza Kwa Viwanda
Na Uwekezaji Mkubwa Nchini Lakini Pasipo Elimu Tutabaki Kuwa Watazamaji Tu Na
Ameeleza Kuwa Anasikitishwa Sana Na Hali Halisi Ya Watu Inapofikia Swala La
Elimu Wengi Wanapeleka Watoto Serikalini Kuwa Ni Yatima Wakati Inapofika Katika
Suala La Unyago Wanauwezo Wa Kuwahudumia Na Kuhudumia Gharama Za Ngoma Hizo Na
Kwanini Washindwe Kwenye Swala La Elimu Pia Alisema Yeye Kama Mkuu Wa Wilaya
Amekuwa Akijitahidi Sana Kutafuta Fursa Kwa Watu Wa Mtwara Ila Zinafeli
Kutokana Namazingira Ya Elimu Ya Wahusika Kuwa Ndogo Kwa Mfano Mwaka Jana AMREF
Ilitoa Pesa Zaidi Ya Shilingi Million Arobaini Kwa Wilaya Ili Waweze Kusomesha
Watoto Waliopata C Tatu Za Masomo Ya
Sayansi Katika Fani Za Uganga Na Uuguzi Lakini Fedha Hizo Zilihamishwa Na
Kupelekwa Bukoba Kwakuwa Mtwara Waliosekana Watu Wenye Sifa Hiyo Iliyohitajika.
Katika Suala Hili
Wanafunzi 35 Wangweza Kusomeshwa Kwa Kulipiwa Ada Zaidi Ya Million Moja Lakini
Pia Kwa Upande Mwingine Alielekeza Lawama Kwa Walimu Wa Masomo Kufanya Bidii
Katika Masomo Yao Kwani Haiwezekani Mwalimu Unafundisha Mwaka Mzima Na Somo
Lako Wanafunzi Wanapata Sufuri Hili Nalo Ni Tatizo La Elimu Kwa Huku Kusini
Hususani Mtwara.
No comments:
Post a Comment