EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, February 19, 2014

RAI: USHIRIKI WA HALI YA JUU KATIKA HILI WAHITAJIKA MTWARA


NA: MWANDISHI WETU
Wananchi wa mkoa wa Mtwara wametakiwa kuwa na utaratibu wa kutoa ushirikiano wa kutosha pindi fursa mbali mbali zinapojitokeza.
Rai hiyo imetolewa na  shirika lisilo la kiserikali la compassion international linaliojihusisha na huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, ambalo limeanza kutoa huduma zake rasmi hivi leo katika maeneo ya raha leo opharnege center mkoani Mtwara.
Akizungumza na wananchi mwezeshaji wa shirika hilo Audats kisato, amesema kuwa wao kama compassion international wameamua kuhudumia jamii ya watu wa mtwara, baada ya kufanya hivyo katika mikoa tofauti nchini kwa lengo la kuikwamua jamii kutoka katika umaskini na hali ngumu ya maisha.
Kisato amesema kuwa shirika hilo lenye makao makuu nchini marekani katika jimbo la Colorado, limefanikiwa kufadhili watoto katika nchi 28 ambazo kati ya hizo 12 ni nchi za afrika,  ikiwemo Tanzania Kenya na Uganda.
Hata hivyo amewatoa wananchi  wasiwasi kwa kueleza kuwa shirika hilo limesajiliwa na kufahamika kisheria, na katika nchi ya Tanzania makao makuu yake yako mkoani arusha,  ambako ndiko waliko anzisha huduma hizo mnamo april mwaka 1999.

No comments:

Post a Comment