WEBBER AAMUA KUACHANA NA LANGALANGA MWISHONI MWA MSIMU.
DEREVA nyota wa
langalanga wa timu ya Red Bull, Mark Webber ameamua kuachana na
mashindano hayo ikifikapo mwishoni mwa msimu huu. Katika
miaka 12 ambayo amekuwa akishiriki michuano ya langalanga Webber ambaye
pia amewahi kuendesha katika timu za Minard, Jaguar na Williams
ameshinda mashindano mbalimbali ya Grand Prix mara tisa na kumaliza
katika nafasi ya tatu katika mashindano ya dunia mara tatu. Akihojiwa
kuhusiana na uamuzi huo Webber amedai kuwa anadhani huo ni wakati
muafaka kwake kuachana na mbio za langalanga na kuangalia mambo
mengine. Msimu
wake mzuri ulikuwa ni mwaka 2010 ambapo aliongoza karibu msimu wote
kabla ya kuteleleza katika mashindano matatu ya mwisho na kushuhudia
dereva mwenzake wa Red Bull Sebastian Vettel na Fernando Alonso wa
Ferrari wakimpita. Dereva
wa Lotus Kim Raikkonen ambaye ni bingwa wa michuano ya dunia mwaka 2007
ndio anapewa nafasi kubwa kuchukua nafasi ya Webber ambaye aliingia
katika langalanga mwaka 2002.
TEVES ATUA JUVENTUS.
KLABU ya Juventus ya
Italia jana ilimtangaza rasmi kumsajili mshambuliaji nyota wa kimataifa
wa Argentina, Carlos Tevez kutoka timu ya Manchester City kwa mkataba wa
miaka mitatu. Taarifa
zinadai kuwa klabu yenye maskani yake katika jiji la Turin wamelipa
kiasi cha paundi milioni 10 kwa nyota huyo mwenye umri wamiaka 29. Lakini
Tevez atatakiwa kumaliza adhabu yake ya kutumikia jamii kwa saa 250 ili
kuondoka jijini London salama na kuepuka kuburuzwa tena mahakamani. Tevez
alikatisha likizo yake huko Amerika Kusini na kupanda ndege kuelekea
Italia jana lakini pia atatakiwa kumaliza adhabu yake aliyopewa na
mahakama ya Macclefield April mwaka huu kwa kuendesha huku akiwa
amefungiwa kufanya hivyo.
KIRUI, KIPSANG WAJITOA MARATHON MOSCOW.
BINGWA mara mbili wa
dunia mashindano ya mbio ndefu Abel Kirui na mshindi wa medali ya shaba
katika michuano ya olimpiki Wilson Kipsang wamejitoa katika timu ya
wanariadha ya Kenya itakayoshiriki michuano ya riadha ya dunia
itakayofanyika jijini Moscow. Makamu
wa rais wa Chama cha Riadha cha nchi hiyo Paul Mutwii amedai kuwa Kurui
aliwafahamisha kwamba amejitoa kwasababu ya kusumbuliwa na majeraha
wakati Kipsang yeye amewaambia kuwa ana majukumu mengine. Kirui
ambaye alishinda taji la dunia la mbio ndefu mwaka 2009 na 2011 amekuwa
akisumbuliwa jeraha la kifundo cha mguu wake wa kulia na anatarajiwa
kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita. Kuziba
nafasi hizo Mutwii amesema wamewaita Mike Kipyego ambaye alishinda mbio
za marathon jijini Tokyo mwaka jana, Bernard Kipyego mshindi wa medali
ya fedha mbio za nusu marathon 2009 na bingwa wa mbio za marathoni za
Paris Peter Some. Kikosi cha mwisho kitakachokwenda Moscow kitatajwa mwezi ujao baada ya kufanyika mbioza mchujo.
BADO SIJAFULIA - FEDERER.
MCHEZAJI tenisi nyota wa
Switzerland, Roger Federer amesisitiza kuwa bado ataendelea kucheza
mchezo huo kwa miaka mingi ijayo pamoja na kutolewa mapema katika
michuano ya Wimbledon jana. Nyota
huyo ambaye anashika namba tatu katika orodha za ubora duniani amesema
hana hofu yoyote pamoja na kutolewa na Sergiy Stakhovisky wa Ukraine
katika mzunguko wa pili wa michuano hiyo. Katika
mchezo huo Federer aliburuzwa kwa kufungwa 6-7 7-6 7-5 7-6 na
Stakhovsky anayeshika namba 116 katika orodha za ubora duniani. Baadhi
ya wadau wa mchezo huo wamekuwa wakihoji kiwango cha Federer mwenye
umri wa miaka 31 na kudai kuwa amekwisha lakini mwenye amesisitiza kuwa
bado yuko fiti na ataendelea kucheza kwa miaka kadhaa ijayo. Kwa
upande wa wanawake mwanadada nyota anayeshika namba mbili kwa ubora kwa
upande wanawake Maria Sharapova wa Urusi naye aliyaaga mashindano hayo
baada ya kukubali kipigo cha 6-3 6-4 kutoka kwa Michelle Larcher de
Brito wa Ureno anayeshika namba 131 katika orodha hizo.
BADO HATUKO FITI KWA KOMBE LA DUNIA - SCOLARI.
KOCHA wa timu ya taifa
ya Brazil, Luis Felipe Scolari amekiri kuwa kikosi chake bado hakiwezi
kuanza kuota kunyakuwa taji lao la sita la Kombe la Dunia mwaka ujao
lakini wamebakisha mechi moja kunyakuwa taji lao la tatu la Kombe la
Shirikisho baada ya kuiengua Uruguay katika hatua ya nusu fainali. Scolari
amesema anafikiri kikosi hicho kimefikia mahali pazuri lakini bado kuna
vitu vingi vya kufanyia marekebisho mpaka kikamilike kwa ajili ya
michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Kocha
huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa wanahamishia nguvu zao katika mchezo
wa fainali na baada ya hapo wataangalia mapungufu yalijitokeza ili
kuhakikisha wanakuwa na kikosi imara kitakachoweza kulibakisha Kombe la
Dunia nyumbani. Brazil
kwasasa wanasubiri mshindi wa nusu fainali nyingine ya michuano hiyo
itakayopigwa baadae leo kati ya mabingwa wa Ulaya na Dunia Hispania
watakaochuana na Italia.
Wednesday, June 26, 2013
RONALDO AZIDI KUWATIA TUMBO JOTO MADRID.
MSHAMBULIAJI nyota wa
kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo anaweza kuwa njiani kurejea
Manchester United kutokana na tetesi kuwa atafanya mazungumzo na
viongozi wa Old Traford katika siku tatu zijazo. Nyota
huyo wa klabu ya Real Madrid amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea
Uingereza baada ya kuonekana kukosa furaha huko Santiago Bernabeu lakini
inaaminika kwamba ujio wa Carlo Ancelotti unaweza kushawishi kubakia
nchini Hispania. Gazeti
moja nchini Hispania liliripoti kuwa Ronaldo ambaye ni nahodha wa timu
ya taifa ya Ureno atakutana na viongozi hao wa United kabla ya kurejea
Madrid kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi. Meneja
mstaafu wa United Sir Alex Ferguson katika kipindi cha karibuni amekuwa
akimfukuzia Ronaldo ambaye inaaminika kutaka nafasi ya kuiwakilisha
klabu hiyo ambayo ndiyo iliyomtengeneza mpaka kuwa mmoja wa wachezaji
bora duniani. Rais
wa Madrid Florentino Perez amenyesha kuwa na uhakika wa nyota huyo
mwenye thamani ya paundi milioni 80 kusaini mkataba mwingine ambao
utambakisha nchini humo lakini Ronaldo alikanusha habari hizo katika
mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment