EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, August 2, 2012

Baada ya Bosi na mmiliki wa clabu ya Azam fc,kutoa tamko kwa uongozi wa klabu yake kuwa ihakikishe inamtoa mchezaji Mrisho Ngasa na kumuuza kwa timu yoyote haraka iwezekanavyo. Kauli hiyo ilitoka mapema baada ya mchezaji huyo (Ngasa) kuonyesha kuwa na mapenzi na timu ya Yanga ya Dsm tukio ambalo lilithibitishwa mara baada ya ngasa kuonekana akiivaa na kuibusu jezi ya yanga muda mfupi baada ya kumalizika kwa mechi ya nusu fainali katika michuano ya kagame uwanja wa taifa mechi ambayo ilichezwa kati ya Azam na As vitar ya kongo na Azam kuibuka kidedea. Mrisho Ngasa ambaye alibakiwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kukipiga Azam, hapo jana imemlazimu kusaini mkataba mpya na Clabu ya Simba ya jijini dsm ingawa lengo la Azam ilikuwa ni kumrejesha mchezaji huyo katika timu aipendayo ya Yanga lakini ilishindikana kwa kuwa Yanga walionekana kusuasua juu ya kumsajili kiungo huyo kwa kutoa pesa chini ya dau lililohitajika hivyo kuipa nafasi Simba kumchukua kwa Tsh ml.25 badala ya ml20 za yanga.

No comments:

Post a Comment