EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, November 27, 2014

MAALIM SEIF:-MAGEREZA HALI MBAYA LAZIMA TUYAWEKE SAWA:

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (pichani), amesema ni jukumu la taasisi zinazosimamia magereza katika eneo la Afrika Mashariki kuweka mazingira bora yatakayoweza kuhakikisha usalama na haki kwa wafungwa na watu waliomo vizuizini.

Maalim Seif alisema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Kanda unaowashirikisha wajumbe kutoka Ethiopia, Mauritius, Kenya, Uganda na Tanzania kujadili usalama magerezani, adhabu mbadala, kutokomeza dawa za kulevya pamoja na maradhi ya Ukimwi uliofanyika mjini Zanzibar.

Alisema kuna kilio kikubwa miongoni mwa mataifa kutokana na kuwapo mazingira yasiyoridhisha katika magereza, hali ambayo imekuwa ni chanzo cha kuvunjwa kwa haki za wafungwa na huchangia watu hao kupata athari za kiafya.

“Dhana yangi ni kuwa nyote mnafahamu hali duni magerezani katika nchi nyingi, hali iliyopo hata vile viwango cha chini vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa kwa haki za wafungwa havifikiwi,” alisema Maalim Seif.

Alieleza kuwa msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza mengi inachangia kukosekana kwa huduma kama vile kupata mwangaza wa kutosha, hewa safi ambapo matokeo yake kiwango cha maradhi ya kifua kikuu na maambukizi ya ukimwi ni ya kiwango cha juu katika sehemu hizo.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment