EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, July 10, 2014

USAJIRI WA SUAREZ WAKAMILIKA NA SASA BARCA YASUBIRI RIDHAA YA FIFA TU KUTANGAZA

KLABU ya Barcelona inatumai kutangaza kumsajili Luis Suarez Alhamisi hii mara tu Alexis Sanchez atakapokamilisha usajili wake Arsenal.

Usajili huo unaweza kuchelewa hadi Ijumaa, wakati wakisubiri ufafanuzi kutoka FIFA juu ya adhabu yake ya miezi mine inayomzuia kujihusisha kabisa na masuala ya soka.
Suarez amefungiwa baada ya kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini wakati Uruguay ikimenyana na Azzuri katika Kombe la Dunia mwaka huu Brazil.
Kwaheri? Luis Suarez anatazamiwa kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 75 kutua Barcelona akitokea Liverpool
Ready for Luis: Futbolmania are already stocking 'Suarez 9' shirts ahead of his expected move to La Liga
Tayari kwa Luis: Barca tayari imekwishaandaa bidhaa za kuuza kwa jina la Suarez atakayepewa jezi namba 9 atakapotua La Liga
Done deal: Arsenal look set to complete the £30m signing of Chile star Alexis Sanchez from Barcelona
Dili imekaa safi: Arsenal inatarajiwa kukamilisha usajili wa Pauni Milioni 30 wa nyota wa Chile, Alexis Sanchez kutoka Barcelona
 Lakini ni baada ya Arsene Wenger kukamilisha uhamisho huo wa Pauni Milioni 30 wa mshambuliaji wa Barcelona, Sanchez, ndipo uhamisho wa Suarez wa Pauni Milioni 75 kuhamia Katalunya utakamilishwa pia.
Nyota wa Chile, Sanchez amechagua kwenda The Gunners badala ya Liverpool na Juventus na wawakilishi wake wapo London kuzungumzia vipengele vya Mkataba binafsi wa mchezaji huyo.
Sanchez anatarajiwa kupewa ofa ya mshahara saws na mchezaji anayelipwa zakidi, Mesut Ozil, ambaye analamba Pauni 140,000 kwa wiki. Arsenal itafika dau la Barcelona la Pauni Milioni 30 ili kuiwezesha timu hiyo ya Hispania kukamilisha usajili wa Suarez.

No comments:

Post a Comment