EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, July 10, 2014

POGBA SASA ATIMKIA CHELSEA KUZIBA PENGO LA FRANK LAMPARD

Meneja wa kiungo Paul Pogba ameeeleza kuwa mchezaji wake huyo anaweza akajiunga na Chelsea kama ilivyoelezwa na kocha mkuu wa klabu hiyo Jose Mourinho, pogba ambaye alionekana kuwa ni mchezaji nyota katika kombe la dunia nchini Brazil akiwa na timu yake ya taifa ya ufaransa ametajwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji vivutio kwa kocha mbwatukaji Mourinho anayeinoa Chelsea ya ncini uingereza na tayari mazungumzo yameanza kufanyika ambapo pogba ameeleza kutamani kuichezea  chelsea kwa lengo la kuziba pengo la Frank Lampard.

WAKATI HUOHUO CHELSEA IMEMSAINISHA KANDARASI mchezaji mwenye umri wa miaka 29 ambaye alikuwa ni miongoni mwa wachezaji 30 waliokamilisha kikosi cha timu ya taifa ya Croatia ambacho kilishiriki kombe la dunia huko nchini brazil naye si mwengine ni MARIO Pasalic ambaye alikua anachezea klabu ya Hajduk split na dili hilo limekamilika jana mchana.Pasalic aliandika kwenye mtandao wa klabu ya Chelsea mara baada ya kusaini mkataba kuwa ana furaha sana kwakua sasa amekua mchezaji wa Chelsea.Na akasema kuwa anawashukuru watu wote wa klabu yake ya zamani ya Hajduk na sasa anaanza maisha mapya ya soka akiwa uingereza.Pasalic atakua anacheza katikati kama kiungo kwa Chelsea akiziba nafasi ya Lampard na amesema anafuraha kuwa mbadala wa Lampard kwakua alikua anampenda sana.

No comments:

Post a Comment