EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, April 14, 2014

KIKWETE ATUHUMIWA BUNGE LA KATIBA ,MKOSAMALI AFUNGUKA JUU YA TUHUMA HIZO

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Felix Mkosamali.PICHA|FILE 


Dodoma. Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Felix Mkosamali (pichani chini), jana alirusha tuhuma kwa Rais Jakaya Kikwete na Spika wa Bunge Muungano, Anne Makinda akidai kuwa ni viongozi vigeugeu kutokana na kutaka mfumo wa serikali mbili.
Kutokana na hilo, Mkosamali alipendekeza wajumbe wote wanaopinga mfumo wa serikali tatu, wabebe mabegi yao na kuondoka bungeni kwa kuwa hawako tayari kuona katiba inatungwa ya CCM pekee.
Alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa mchango wake kwenye Rasimu ya Katiba katika Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ambayo wajumbe walianza kuchangia jana.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta alimtaka mjumbe huyo kufuta kauli yake ya viongozi vigeugeu ili kupunguza kelele za wajumbe ambao walianza kuzomea kuwa alikuwa anakiuka kanuni.
Mkosamali ambaye ni Mbunge wa Kibondo (NCCR-Mageuzi), alisema kuwa nchi ya Tanzania haitasonga mbele kutokana na kuongozwa na watu ambao ni vigeugeu.
Aliwatuhumu viongozi hao kuwa wamekuwa wakitenga fedha nyingi kwa ajili ya kufanya propaganda za kulipana posho huku wakilitupa na kulisahau Azimio la Arusha ambalo lilikuwa na maadili mema.
Alisema wanachokifanya wajumbe wa CCM ni kupuuza maoni ya Tume ya Jaji Joseph Warioba ili waendelee kutengeneza Katiba ya kukaa mahali na kulipana rushwa.
“Mnajifungia ndani watu wawili mnaandika maoni yenu kisha mnaleta yanakuwa ni maoni ya kukariri, mnapopuuza maoni ya wananchi kwa serikali tatu, hizo mbili mlipata maoni ya watu gani?” alisema.
Mapema jana Asha Bakari Makame, nusura achafue hali ya hewa bungeni wakati akichangia kwenye rasimu hiyo baada ya kuanza kumshambulia Ismail Jussa kwamba analazimisha muundo wa serikali tatu ambao hautawezekana.
SOURCE>>>>>MWANANCHI

No comments:

Post a Comment