EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, February 6, 2014

MKUU WA WILAYA ANUSURU SHULE KUFUNGWA KWA NJAA MTWARA

NA : KASSIM NGUMBI
Mkuu Wa Wilaya Ya Mtwara Ameanza Shughuli Ya Ugawaji Wa Mahindi Ya Msaada Kwa Kata Mbalimbali Za Halmashauri Ya Mtwara Vijijini Ili Kukinga Hali Mbaya Inayowza Kujitokeza Wakati Wowote Ya Wananchi Kukosa Chakula Kutokana Na Hali Ya Hewa Kutokuwa Mzuri Na Kupelekea Baadhi Ya Mzao Yaliyoko Mashambani Kama Vile Mahindi  Kuanza Kukauka Huku Ayakiwa Tayari Yalifikia Katika Hatua Ya Kukarbia Kuliwa Nah Ii Inatokana Na Hali Ya Kutokuwepo  Kwa Mvua Ndani Ya Msimu Huu Wa Masika Mkoani Mtwara.
SWACOTZ FORUM Ilishuhudia Hali Ya Mashamba Mbalimbali Ilivyo Huko Vijijini Wakati Ilipotembelea Maeneo Mbalimbali Ya Mtwara Vijijini Mwishoni Mwa Wiki Iliyopita Kaa Vile Eneo La Kivava Boda Ambako Ni Mpakani Mwa Tanzania Na Msumbiji Pamoja Na Kitaya,Mahurunga Na Kitere N Kushuhudia Hali Ya Mahindi Yaliyokauka Na Mazao Mengine Lakini Pia Mwandishi Wa

Habari Hii Alipofika Katika Kata Ya Njengwa Wananchi Walimweleza Hali Halisi Iliyoko Katika Maeneo Hayo Ambapo Kwakweli Hali Ni Mbaya Ambapo Moja Ya Wananchi Hao Aliyejitambulisha Kwa Jina Moja La Rehema Salum Ambaye Pia Ni Mzazi Wa Watoto Watatu Alisema Kuwa Katika Hali Isiyo Ya Kawaida Na Haijawahi Tikea Mwaka Huu Imeonekana Kuuuandama Mkoa Wa Mtwara Kwa Mazao Kukauka Kutokana Na Jua Kali Linaloendelea Kuwaka Kila Siku Zinaposogea Baadhi Ya Sehem Mazao Yalionekana Kuja Vizuri Na Kufikia Hatua Ya Kuleta Tumaini La Kuliwa Kwa Mfano Mahindi Tayari Yameanza Kuchanua Na Mengine Kubeba Magunzi Lakini Jua Limeanza Kuwaka Mfululizo Na Kupelekea Mazao Hayo Kuanza Kukauka Huku Wananchi Wakiwa Hwana Chakula Na Hawajuwi Nini Cha Kufanya Aidha Mwanamke Huyo Alisema Kuwa Wao Katika Kijiji Chao Cha Chihwindi Kilichopo Kata Ya Njengwa Almashauri Ya Mtwara Vijijini Mkoani Mtwara Tayari Wameanza Mikakati Ya Kuangalia Uwezekano Wa Kuifunga Shule Ya Msingi Iliyoko Katika Eneo Lao Kutokana Na Haloi Kuzidi Kuwa Mbaya Kwani Watoto Wamekuwa Wakishindwa Kusoma Kutokana Na Njaa Na Badala Yake Wengi Wanaishia Vichakani Kuchuma Matunda Poli Na Kuyala Wakati Ambao Walitakiwa Kwenda Shuleni, Pia Alieleza Kuwa Hali Hiyo Inasababisah Hata Wananchi Wenyewe Kukata Tama Ya Kufanya Maandalizi Ya Mashamba Mapya Kwa Ajili Ya Kilimo Cha Msimu Wa Kiangazi
“Tumeishiwa Baba Hali Ni Mbaya We Si Unaona Mwenyewe Mahindi Yote Yamekauka Kwa Jua Hapa Tunawaza Kuifunga Shule Ili Watoto Wakae Nymbani Sababu Ya Njaa” Alisema Mama Huyo Akimuelezea Mwandishi Wa Habari Hizi Lakini Wakati Haya Yakiendelea Serikali Ya Wilaya Ya Mtwara Kupitia Mkuu Wake Wa Wilaya MH: Wilman Kapenjama Ndile Tayari Imeanza Kusambaza Mahindi Ya Msaada Kutokea Kwenye Mfuko Wa Maafa Na Mahindi Hayo Yanasambazwa Kwenye Kila Kata Ili Kuzisaidia Kaya Za Maeneo Husika Mara Baada Ya Kugundulika Kuwepo Kwa Hali Mbaya Ya Hewa Inayosababisha Kupotea Kwa Mazao Yaliyoko Mashambani.Mahindi Hayo Yatakuwa Yakiuzwa Shilingi 50 Kwa Kilo Mojha Na Kila Kaya Itapata Kulingana Na Mpangilio Uliopangwa.  Lakini baadhi ya viongozi tayari wameanza kuzungumza na makundi mbalimbali ya wananchi na kuwashauri kulima vilimo mbadala kama vile ufuta na huku muhogo ukipewa kipaumbele na kuonekana kuwa ni kilimo pekee kitakachoikomboa mtwara kwa mwaka huu kutokana na kuvumilia hali ya ukame.

MBUNGE WA CHADEMA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki (Chadema), Sylvester Kasulumbayi.PICHA|MAKTABA 
Na Shija Felician, Mwananchi

Kahama. Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki (Chadema), Sylvester Kasulumbayi na Diwani wa Kata ya Buselesele, Crispian Kagoma na watu wengine 14 wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kujeruhi katika vurugu zilizoibuka katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kasulumbayi na wenzake 15, ambao wanaaminika kuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama saa 8.00 mchana jana na kusomewa mashtaka sita kila mmoja.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Gadiel Mariki, Mwendesha Mashtaka Shukrani Madulu alisema washtakiwa wote kwa pamoja walitenda makosa hayo Februari 4, mwaka huu.
Madulu aliiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao wakiongozwa na mbunge huyo walitenda kosa hilo la kuwashambulia kwa mapanga wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za kuwania udiwani wa Kata ya Ubagwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.
Alisema mashtaka matano ni kushambulia na kujeruhi kwa mapanga, na moja la kuharibu mali, ikidaiwa kuwa katika vurugu hizo washtakiwa waliishambulia gari la CCM la wilaya hiyo na kuliharibu.

Washtakiwa wote walikana mashtaka yote na kuomba mahakama iwape dhamana ili waendelee na kampeni za kumnadi mgombea wao wa nafasi ya udiwani katika kata hiyo ya Ubagwe.
Maombi hayo yalipingwa na Mwendesha Mashtaka, akiiomba mahakama isitoe dhamana kwa kuwa hali za majeruhi watatu ni mbaya kwa kuwa tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Rufaa na Bugando mkoani Mwanza, baada ya matibabu yao kushindikana wilayani Kahama.
Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mariki alikubaliana na hoja hiyo na kuahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo kesi hiyo itasikilizwa.
Watuhumiwa wote walipelekwa mahabusu baada ya dhamana hiyo kuzuiliwa.
Waliojeruhiwa kwenye vurugu
Wafuasi watano wa CCM wilayani Kahama akiwamo ofisa mtendaji wa Kata ya Ubagwe walijeruhiwa kwa mapanga kwenye vurugu hizo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Andrew Emmanuel alisema Masunga, Kamaro na Peter walisafirishwa kwenda Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment