EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, February 26, 2014

HUU NDITO UKWELI KUHUSU MATESO YA DK. CHENI NA FREEMASON

MINONG’ONO na uvumi unaotambaa kwa kasi kuwa anajihusisha na taasisi ya wajenzi huru (Freemasons), unazidi kumtesa msanii wa filamu za Kibongo, Mahsein Awadhi Said ‘Dk. Cheni’ kwa madai ya kwamba anajisikia vibaya anaponyoshewa vidole na baadhi ya wadau wa tasnia hiyo.
 
Dk. Cheni.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mwandishi wetu alisikia fununu kutoka kwa wadau wengi wa filamu wakiwemo wasanii wenzake wakidai  kuwa Dk. Cheni ni mwanachama halali wa taasisi hiyo ndiyo maana mambo yake ni mazuri kifedha ukilinganisha na wasanii wengine wanaoaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuigiza kuliko yeye.
“Kila dalili inaonesha kabisa Dk. Cheni ni Freemason, angalia mavazi yake mengi ni meusi, machata na alama kibao zinazohusishwa na taasisi hiyo, angali fedha aliyonayo, angalia hata gari lake lilivyojaa alama za ajabu ajabu, huyu jamaa ni Freemason kabisa,” alisema mdau mmoja wa filamu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alipozungumza na mwandishi wetu.
Kauli kama hizo zimekuwa zikitolewa kwa nyakati tofauti na baadhi ya wasanii wenzake.
Dk. Cheni alipotafutwa kwa njia ya simu Jumapili ya wiki iliyopita na kuulizwa madai hayo alikuwa na haya ya kusema:

“Dah! na wewe umeyapata kaka? Hakika naumia sana na madai hayo, yamevuma sana kwa wadau, tena baadhi yao ni watu ninaowaheshimu sana, jamani mimi siyo Freemason, naigiza, kazi zangu za u-MC zinaniingizia kipato, najiwekea akiba.
“Si mtu wa starehe, nawekeza katika biashara ndogondogo, madai haya ya Freemason yananitesa sana ila namwachia Mungu,” alisema Dk. Cheni.

No comments:

Post a Comment