NA: KASSIM NGUMBI
Kaya Thelathin
Na Saba Za Vijiji Vine Vya Kata Ya Nanyamba Katika Halmashauri Ya Mji Mdogo Wa
Nanyamba Zimejikuta Zikiingia Katika Hali Ya Sintofaham Na Baadhi Kukosa Mahali
Pa Kuishi Baada Ya Nyumba Walizokuwa Wakiishi Kubomolewa Na Mvua Iliyoambatana
Na Upepo Mkali Ambayo Imenyesha Usiku Wa Kuamkia Leo.
Akizungumza Katika
Ofisi Ya Kata Ya Nanyamba Mbele Ya Wahanga Wa Tukio Hilo Mkuu Wa Wilaya Ya
Mtwara Mh: Wilman Kapenjama Ndile Aliyekuwa Ameambatana Na Mkurugenzi Mtendaji
Wa Halmashauri Ya Wilaya Mtwara Vijijini Katika Ziara Ya Kuwapa Pole Wahanga
Hao Alisema Kuwa Serikali Imepokea Kwa Masikitiko Makubwa Taarifa Za Tukio Hilo
Zilizotolewa Na Diwani Wa Kata Hiyo
(Ccm) Mh: Mmauji Na Ndioyo Maana
Imefika Kuwatembelea.
Aidha Mkuu
Huyo Wa Wilaya Aliwataka Wananchi Kuwa Na Subra Katika Kipindi
Hiki Na Wale
Ambao Numba Zao Zimeharibika Kabisa Basi Wajishikize Kwa Ndugu Na Jiran Huku Serikali Ikiangalia Namna Ya Kuwasaidia
Ingawa Hakusema Iwapo Watu Hao Wangesaidiwa Gharama Za Ujenzi Licha Ya Kuahidi
Kuwapatia Msaada Wa Chakula Ifikapo Jumanne Ijayo Ya Tarehe 21 Mwezi Huu.
Katika Safari
Yake Mkuu Wa Wilaya Alitembelea Maeneo Yaliyotokea Matukio Hayo Na
Kujionea Maafa Makubwa Yaliyoachwa Na
Mvua Hizo Ikiwamo Kubomolewa Kwa Makazi Ya Watu Pamoja Na Uharibifu Wa Mimea Ya
Mazao Kama Vile Mikorosho.
Hata Hivyo
Hakuna Mtu Aliyeripotiwa Kujeruhiwa Wala Kufariki Dunia Mpaka Sasa Kutokana Na
Tukio Hilo Hali Inayopelekea Wakazi Wa Eneo Hilo Kumshukuru Mungu Kwakuwa Wote
Wameweza Kunusuruika Kwa Upande Wake
Diwani Wa Kata Hiyo Mh, Mmauji Alieleza Tukio Hilo Kuwa Si Lakawaida Kwani Haijawahi Tokea Kwa Kipindi
Cha Hivi Karibuni Huku Akimshukuru Mkuu Wa Wilaya Na Mkurugenzi Kwa Kuja Haraka
Kujionea Na Kuwapa Pole Wananchi Hali Ambayo Itarejesha Matumaini Kwa Wananchi
Hao.
No comments:
Post a Comment