Tuesday, June 11, 2013

NEYMARANAHITAJI KUPEWA NAFASI ZAIDI BARCA

TITO VILANOVA AMUACHE NEYMAR ANG'ARE - YASIWE YALEYALE YA GUARDIOLA KWA SANCHEZ


Mapinduzi mapya ya klabu ya Barcelona yameanza rasmi. Neymar, mchezaji kinda mwenye soko kubwa katika dunia ya soka hatimaye amehamia barani ulaya.  
 Kumekuwepo na wasiwasi juu ya kupanda kwa kiwango chake katika mika hii mwili iliyopita, tofauti na wakati alivyokuwa akiibuka.

Kusita kwake (au kushariwa na washauri/wawekezaji wake) kuhamia ulaya mapema kumeleta tatizo katika maendeleo yake ya uwanjani. Lakini sasa tutakwenda kushuhudia uwezo wake halisi wiki kwa wiki. Huku wengi wakimfananisha Neymar na Ronaldinho ambaye alileta mapinduzi makubwa alipojiunga na klabu ya Catalunya muongo mmoja uliopita. Lakini je Barca ya sasa ni mahala sahihi kwa mchezaji aina ya Neymar? 

Funzo la Alexis Sanchez 


Alexis Sanchez alikuwa akionekana mchezaji mwenye 'future' nzuri kwenye ulimwengu wa soka miaka kadhaa iliyopita. Alikuwa akisakwa na karibia na vilabu vyote vikubwa barani ulaya na hakuweza kukataa kujiunga na Barcelona. Hii ilikuwa baada ya msimu wa 2010/11, ambao tulishuhudia Barca ikicheza soka lilowafanya kuwa timu ya kipekee katika ulimwengu wa soka. Lilikuwa jambo gumu kuufuata msimu ule. Jaribio la kuchukua uamuzi wa kuiongezea umahiri au kubadili staili ili kuendelea kutawala soka lilikuwa gumu

Guardiola akaendeleza mtindo wa ‘tiki-taka’ mbele zaidi, akikijaza kikosi cha viungo wengi na kuharibu balance ya timu. Ingawa mwanzoni alipata mafanikio baada ya kushinda Kombe la dunia la vilabu Dec 2011 na baada ya hapo mambo yakaanza kwenda mlama kwa Barca na Guardiola.

Wachezaji wapya Fabregas na Sanchez ambao walianza vizuri sasa wakaanza kupata taabu kuweza kuzoea mfumo wa Guardiola. Viwango vyao vilianza kushuka kwa sababu kama alivyosema kwamba 'kuichezea Barca ni kama kujifunza tena soka.” 

Kutokana na kushuka kwa viwango vya wachezaji wapya, pia kumtegemea zaidi Lionel Messi, na labda kukosekana kwa David Villa kwa sababu ya majeruhi. Hatimaye kwa bahati mbaya wakaondolewa na Chelsea kwenye nusu fainali ya Champions league - ikaonekana wazi kudondoka kwa utawala wa Barca.

Wakati Guardiola na bodi ya Barca ilitaka kuhakikisha falsafa ya Pep inadumu na kuendelea. Vilanova akapandishwa kuwa kocha mkuu - uamuzi ulipaswa kuwa sahihi. Lakini ulikuwa sio mzuri kwa maendeleo ya Barca. Ingawa Barca walionekana imara mwanzoni mwa msimu, kipigo cha kwenye Super cup kutoka Madrid kilionyesha tena udhaifu wao. Vilanova alihitaji kufanya usajili mzuri ili kukiongezea uimara kikosi chake na badala yake akamnunua Alex Song ambaye anahitajika kwa wakati huo.

Wakati Vilanova alipogundulika kwa mara nyingine kusumbuliwa na kansa timu ilionekana wazi kuathirika hasa alipoondoka kwenda kupata matibabu. Michezo ambayo alikuwa hayupo iliifanya Barca kuonesha udhaifu wake jaokuwa ukweli ni kwamba timu kama Madrid, PSG, na hatimaye Bayern zilishajifunza namna ya kucheza na Barca na kuwafunga. Hata Milan waliweza kuisimamisha kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya mtoano. Namna yao ya uchezaji na hasa labda katika kumtegemea Messi kuliwafanya Barca kutabirika.

Mabadiliko ya mfumo
 

Usajili wa Neymar ulikuwa muhimu kwasababu unatoa ahadi kutoa kitu kingine cha tofauti tangu usajili wa David Villa. Villa alianza vizuri na jukumu la kucheza mshambuliaji wa pembeni lakini akaanza kuhisi kutengwa baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya wanacatalunya. Neymar anaonekana ni mtu anayeweza kutoa suluhisho kwenye nafasi ya Villa na kuipa Barca muelekeo mpya.

Ingawa, funzo la Alexis Sanchez mpaka kwa Zlatan  linaonyesha tatizo ambalo ni lazima lishughulikiwe. Sanchez na Fabregas wote wamehangaika kuuzoea mfumo wa Barca ambao umewafanya wachezaji wazuri sana kuonekana wa kawaida. 

Hawa sio wachezaji wabaya kabisa lakini mfumo ambao wameambiwa wautumikie sio mzuri kwa upande wao. Ukweli ni kwamba utegemezi mkubwa wa mazao ya La Masia ni mzuri na kuigwa kwa mafanikio waliyoyapata Barca, lakini mbinu zao zipo 'complex' sana kwa wachezaji wengi kuzielewa bila kuharibu staili yao ya uchezaji na hata wachezaji wa daraja la juu duniani kutoka nje ya wanapata taabu kuuzoea mfumo huo. Hii sio nzuri kwa hatma ya mbele ya Barcelona.

 Puyol, Iniesta, Pique, Xavi, Villa, Alves na Valdes wote wanakaribia kufikia kilele cha soka lao pale Barca, kizazi kipya kinahitajika kujaza nafasi zao. Hili kundi kwa pamoja ndio ulikuwa msingi wa mfanikio ya Barca chini ya Guardiola ambao aliwatumia Messi na Busquets pia kuitengeneza na kuiboresha staili ya Barca. Sasa mabadiliko yanahitajika na kwa mfumo uliopo inakufanya ujiulize ni kwa urahisi gani wachezaji wanaokuja kujaza nafasi zao watafiti ndani.

Kwa timu yoyote, mageuzi na mabadiliko ni jambo chanya. Bila mabadiliko inaamanisha kutoendelea na kutoendelea kunamaanisha kurudi nyuma. Na siwezi kuacha kufikiria kwamba Barcelona wamekuwa wamesimama kimaendeleo ndani ya dimba kwa miaka miaka 2 sasa. 

Neymar anawakilisha mabadiliko lakini bado yeye pekee hawezi kuiimarisha staili ya timu. Neymar ana-enjoy kucheza huru, na ingawa ameonyesha ana uwezo wa kucheza pembeni kushoto na kuingia ndani lakini pia anapenda kuzunguka kwenye pembe tofauti za uwanja. Hii inaweza nzuri kwa kuifanya Barca kutotabirika lakini bado ataweza kupewa uhuru huo ndani ya Barca?

Wakati Ronaldinho alipowasili Barca alileta hali ya uhai mpya kwenye timu baada ya miaka kadhaa ya kutaabika kwa klabu hiyo. Aliifanya Barca kupata mafaniko makubwa na kuipa ladha ya kuwatazama iliyopotea.

Neymar anawakilisha mwanzo ule ule kama wa Dinho. Ana umri mdogo, mtundu uwanjani, ana akili ni aina ya mchezaji ambaye Barca wanahitaji - baada ya tiki-taka timu inahitaji kurudi kwenye ule mfumo wa kidachi wa 4-3-3 wa total football. Mabadiliko ya mfumo yanahitajika hivyo hilo linamaanisha pia mabadiliko ya kocha.

Muda wa mabadiliko ya kocha

Ili jambo hili liwezekane inabidi Tito Vilanova aondolewe kwenye benchi la ufundi. Ugonjwa wake pekee unamaanisha unaamanisha inabidi asiendelee kufundisha na kufanya kazi ya daraja la juu, yenye stress nyingi. Lakini bado kwenye upande wa soka na falsafa zake, kwa bahati yupo zaidi kama kama Guardiola.

Wakati Guardiola alipojiuzulu labda lilikuwa jambo zuri kwa klabu, jaokuwa ile miaka ya mafanikio ilimfanya awe na thamani na mwenye kuheshimika sana kiasi hivyo labda kwa ushauri wake ikabidi mabosi wa Barca wamfanye msaidizi wake awe bosi mpya. Huu ulikuwa uamuzi m'baya.

Tangu wakati wa Cryuff, mafaniko ya Barca ambayo ingawa sio mara zote yamekuwa na maamuzi ya kufanya mabadiliko na mageuzi kwa wakati sahihi. Cruyff alikuja na staili yake ya ufundishaji ambayo imekuwa alama ya Barca - lakini hawa makocha wa sasa walikuja na kuifanyia maboresho staili ile.

Zama za Guardiola/Vilanova zimekuwa za mafaniko sana kwenye historia ya Barca, lakini historia inatuambia hata kitu kiwe kizuri vipi bado siku moja kitahitaji mabadiliko/maboresho ili kuendelea mbele zaidi. Hapa ndipo walipo Barcelona sasa - baada ya mfumo wa Guardiola kuzaa matunda mengi sasa umefika muda mabadiliko/maboresho ili klabu hiyo iweze kuzidi kusonga mbele.
Kuna makocha wawili ambao watakuwa machaguo sahihi kwa zama za mpya za Barcelona. Kwanza Frank De Boer, kocha mkuu wa Ajax. Mchezaji huyu wa zamani wa Barca anaijua na anajua falsafa ya Ajax/Cryuff vizuri kuliko watu wengi katika ulimwengu wa soka. Hii Ajax yake imefanya makubwa sana ukizingatia na uwezo wao wa kifedha na ameonyesha kwamba anaweza kufundisha katika soka la kisasa. De Boer angekuwa mtu sahihi wa kuipeleka Barca mbele.
Laudrup enzi zake

Kama ambavyo ingekuwa kwa Michael Laudrup. Kwa watu wengi Laudrup amekuwa akitazamwa kama kocha ajaye wa Barcelona. Akiwa na Swansea (Swanselona) ameonyesha wazi anao uwezo, sifa pamoja staili, vitu vinavyomfanya kuwa sifa sahihi za kuwa chaguo mojawapo la kuwa kocha wa Barca. Huyu alikuwa ni mchezaji tegemezi wa Barca wakati wa utawala wa Cruyff wakati wa miaka ya 90 hivyo anaijua vizuri klabu hii.

Wanaume hawa waili wanaijua klabu kiundani pamoja na utamaduni wa soka a klabu hiyo ya Catalunya, na muhimu zaidi wamekuwa mbali na timu kwa miaka mingi sasa. Tatizo ambalo linamkumba Vilanova ni kwamba amekuwa mtu aliyetoa mchango mkubwa na sehemu ya mafaniko ya Barca tangu mwaka 2008. Hiyo ni miaka mitano, na huu utakuwa wa sita kama sehemu ya manejimenti ya timu. Kwa timu nyingi hii ni miaka mingi sasa - na pia bado anawakilisha zama za Guardiola.
Ni muda wa Vilanova kukaa pembeni na kutoa nafasi kwa kocha mpya kuja na kuifanyia mageuzi chanya timu na staili yake. Move ya kurudi kwenye mfumo wa 4-3-3 utawaruhusu wachezaji aina ya Messi, Neymar, Sanchez na Fabregas kung'ara zaidi. Xavi anaweza kuwa mrithi wa Xavi na huku kukiwepo na ongezeko zuri kwenye nfasi ya ulinzi timu inaweza kuanza zama mpya za utawala kwenye soka katika historia ya soka.

Wakati Guardiola alipoingia kwenye uongozi wa benchi la ufundi alirudisha nidhamu ya mpira, akarudisha hali ya kujiamini na kuunda mfumo mpya wa timu ulioleta mafaniko makubwa.


Kwa mara nyingine tena baada ya miaka 5, mabadiliko yanahitajika ili timu izidi kupiga hatua mbele. Neymar anatoa mwanya wa hatua ya kwanza mabadiliko, lakini pia kocha mpya atakuwa jibu la mafanikio ya Barca katika miaka mingi ijayo.

UPINZANI LIGI ZA ULAYA: BARCELONA NA UTAWALA WA KIPEKEE KWENYE LIGI ZA NYUMBANI BARANI ULAYA - LIGI YA UFARANSA YATIA FORA MABINGWA 6 TOFAUTI KATIKA MIAKA 6

Tito Vilanova, Jordi Roura na Aureli Altimira wamesema kabla kwamba ubingwa huu wa ligi haujawa sio wa kwanza kwao, bali wa nne, kwa kuwa wamekuwa na timu hii tangu mwaka 2008 na wakaunda safu ya ukocha iliyosaidia Barca kubeba ubingwa misimu wa 2008/09, 2009/10, 2010/11  – ikiwa ndio timu pekee kufanya hivyo ndani ya miaka mitano iliyopita ikiukosa ubingwa huo kwa msimu wmmoja tu  2011/12.

England, Italia na Ujerumani
Utawala wa Barca kwenye ligi ya nyumbani ni wa kipekee kwenye ligi zote kubwa barani ulaya: Manchester United walishinda ubingwa mara 3 katika miaka mitano iliyopita - Chelsea na Man City wakichukua miaka mingine miwili. Inter, AC Milan na Juventus wote walishinda makombe ndani ya miaka 5 iliyopita ndani Serie A, wakati Bayern Munich na Borrusia Dortmund waligawana utawala Bundesliga.

Porto - Ureno
Kumekuwepo utawala kama wa Barca nchini Ureno, wakati kukiwepo na upinzani wa jadi baina ya Porto na Benfica lakini katika kipindi cha miaka 5 iliyopita ubingwa umekuwa ukipambwa zaidi na rangi za bluu, Porto wamebeba ubingwa mara nne wakati Benfica wakichukua mara tu (2009/10).

Mabingwa sita tofauti ndani ya miaka 6 nchini Ufaransa
Katika ligi nyingi ndogo kumekuwepo na utawala kama Barca - Denmark na Ugiriki, huku  Olympiakos na Copenhagen wakitawala, ligi nyingine kama za Uholanzi, Russian au Turkish, ubingwa umekuwa hauna mwenyewe, timu zimkuwa zikibadilishana. Lakini ligue 1 - Ufaransa hakuna timu iliyotawala ligi katika miaka 6 iliyopita. Katika miaka 6 kumekuwepo na mabingwa sita tofauti. 


No comments:

Post a Comment