Friday, June 7, 2013

HABARI KWA KINA.........MSIBA WA MUME WA HADIJA KOPA NA MAZISHI YA MANGWEA MORO VYAWAFUNIKA WATANZANIA KWA SIMANZI

TASWIRA KUTOKA MSIBANI KWA MAMA MZAZI WA JAFFARI ALLY (MUME WA KHADIJA KOPA)

 Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, akilia kwa uchungu nyumbani kwake Tandale jijini Dar.  Simanzi na majonzi vilitawala msiabani hapo. Akina mama waliofika kumpa pole Mama Mzazi wa Jaffari. SIMANZI, vilio na majonzi vilitawala nyumbani kwa Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, Tandale jijini Dar.  Marehemu Jaffari ambaye alikuwa ni mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa amefariki dunia usiku wa kuamkia jana  katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.  Marehemu Jaffari alikuwa Diwani wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati mama yake...
TUPE MAONI YAKO

KHADIJA KOPA AKIELEKEA UWANJA WA NDEGE JANA KWA AJILI YA MSIBA WA MUMEWE JAFFARI ALLY

Khadija Kopa akilia kwa uchungu mara baada ya kupata taarifa za mumewe kufariki. Akipewa sapoti wakati akielekea uwanja wa ndege. Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar Kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jaffari Ally Yussuf aliyefariki dunia jana alfajiri. Bi Khadija Kopa alikuwa akitokea kwenye maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa juzi....
TUPE MAONI YAKO

HATIMAYE NGWEA AZIKWA KWENYE MAKABURI YA KIBONDA MKOANI MOROGORO....HIZI NDIO PICHA ZA MAZIKO YAKE

Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair leo amezikwa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao. Kabla ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili wake kwenye uwanja wa Jamhuri.    Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika Kusini, wiki iliyopita. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao wamehudhuria mazishi hayo.“Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa sana ni umati usioelezeka mungu akulaze mahali pema peponi,” ameandika Izzo B kwenye...
TUPE MAONI YAKO

PICHA ZA M 2 THE P AKILIA KWA UCHUNGU WAKATI WA KUMUAGA ALBERT NGWEA MOROGORO MCHANA HUU

M2  THE P amefanikiwa  kutoa  salamu zake  za  mwisho  kwa  rafiki yake  kipenzi  ambaye  alikuwa  naye  huko  Afrika  kusini  tena  walikuwa  ndani  ya  chumba  kimoja  kabla ya  mauti  kumkuta Ngwea....!! Mwanzoni, M 2 THE P alikuwa  amefichwa  na  kudanganywa  kuwa  Ngwea  alikuwa  ametangulia  Tanzania. Baadaye  Maggie  alilazimika  kumweleza  ukweli...... ...

No comments:

Post a Comment